IRGC: Kwa uwezo wake mkubwa, Iran itapita kipini cha vitisho na vikwazo
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53894-irgc_kwa_uwezo_wake_mkubwa_iran_itapita_kipini_cha_vitisho_na_vikwazo
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa na kusema: "Mapambano au muqawama na kusimama kidete taifa la Iran ni nukta ambazo zitavunja njama za adui."
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 03, 2019 06:10 UTC
  • IRGC: Kwa uwezo wake mkubwa, Iran itapita kipini cha vitisho na vikwazo

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limetoa taarifa na kusema: "Mapambano au muqawama na kusimama kidete taifa la Iran ni nukta ambazo zitavunja njama za adui."

IRGC imetoa taarifa kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 30 wa kuaga dunia Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na kusema: "Kwa kuwa macho na kwa uwezo wake, Iran itaweza kupita kipindi cha vikwazo na vitisho."

Taarifa hiyo ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu imesema: "Pamoja na kuwepo njama za maadui, Uislamu unazidi kupata nguvu na kustawi duniani."

Imam Ruhullah Khomeini MA

Kesho Jumanne, 4 Juni 2019 sawa na 14 Khordad 1398, utakuwa mwaka wa 30 tokea alipoaga dunia Imam Khomeini MA, muasisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.