Iran na Korea Kusini zasisitizia kutatua matatizo ya kibenki kati yao
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i53912-iran_na_korea_kusini_zasisitizia_kutatua_matatizo_ya_kibenki_kati_yao
Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini amekutana na Gavana wa Benki Kuu ya Iran na kusisitizia umuhimu wa kuzidishwa uhusiano wa pande mbili na kufanya jitihada zaidi kwa ajili ya kutatua matatizo ya kibenki.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jun 04, 2019 13:08 UTC
  • Iran na Korea Kusini zasisitizia kutatua matatizo ya kibenki kati yao

Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini amekutana na Gavana wa Benki Kuu ya Iran na kusisitizia umuhimu wa kuzidishwa uhusiano wa pande mbili na kufanya jitihada zaidi kwa ajili ya kutatua matatizo ya kibenki.

Gavana wa Benki Kuu ya Iran Abdolnaser Hemmati amekutana na Hong Nam-ki, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini ambapo kwa pamoja wamesisitiza kwamba siasa za Marekani za kuiwekea Iran mashinikizo zaidi zimefeli na kwamba serikali za Seoul na Tehran hazipo tayari kuona vikwazo na mashinikizo hayo ya Washington dhidi ya Iran vinavuruga mahusiano ya pande mbili.

Kwa upande wake Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini sambamba na kuashiria sera za Benki Kuu ya Iran katika kipindi cha miezi 10 iliyopita kwa ajili ya kuimarisha hali ya uchumi nchini hapa, amezitaja siasa hizo kuwa hatua muhimu.

Abdolnaser Hemmati, Gavana wa Benki Kuu ya Iran

Kadhalika Hong Nam-ki amesisitiza kwamba Korea Kusini imechukizwa na hali mbaya iliyojitokeza katika uhusiano wa kibenki wa nchi mbili na kadhalika matatizo yaliyowapata wafanyabiashara wa Korea na Iran kufuatia vikwazo na mashinikizo ya Marekani dhidi ya Tehran. Hata hivyo amesisitiza kwamba, kwa kuzingatia kuwa Tehran na Seoul zina uhusiano muhimu hivyo pande zote zinafanya juhudi kwa ajili ya kuondoa matatizo hayo.