Zarif: Siasa za Marekani zimezilenga nchi zote
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54012-zarif_siasa_za_marekani_zimezilenga_nchi_zote
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria siasa haribifu za Marekani na kusisitiza kuwa siasa hizo si tu kuwa zinailenga Iran pekee bali zinazigusa nchi zote.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 09, 2019 03:24 UTC
  • Zarif: Siasa za Marekani zimezilenga nchi zote

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria siasa haribifu za Marekani na kusisitiza kuwa siasa hizo si tu kuwa zinailenga Iran pekee bali zinazigusa nchi zote.

Muhammad Javad Zarif amesema kuwa aghalabu ya nchi zimejiweka kando na siasa hizo za upande mmoja za Marekani na kwamba Marekani inaishinikiza Iran kutokana na udhaifu na kuchanganyikiwa kwake (Marekani). Amesema, pamoja na hayo lakini Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hatimaye itavuka kwa mafanikio mashinikizo yote hayo. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amegusia pia uamuzi wa China na  Russia wa kuacha kutumia sarafu ya dola katika mabadilishano yao ya kiuchumi na kueleza kuwa siasa za kivita zinazotekelezwa na Marekani zimeiathiri dunia na kwamba zinapasa kukomeshwa.

Vikwazo vya Marekani dhidi ya Iran

Zarif amejibu madai ya Brian Hook Mkuu wa Kundi la UChukuaji Hatua dhidi ya Iran katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani kwamba uwezo wa kiulinzi na wa makombora wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ni wa kubuni kwa kusema, "tutaona na msema kweli."