Korea Kusini yaitaka Marekani iiondolee vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54045-korea_kusini_yaitaka_marekani_iiondolee_vikwazo_jamhuri_ya_kiislamu_ya_iran
Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini ameitaka serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 11, 2019 00:49 UTC
  • Korea Kusini yaitaka Marekani iiondolee vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran

Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini ameitaka serikali ya Marekani kuiondolea vikwazo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kim Dong-yeon ameyasema hayo wakati akizungumza na Steven Mnuchin, Waziri wa Fedha wa Marekani ambapo ameitaka serikali ya Washington kuiondolea vikwazo Tehran kwa lengo la kushirikiana zaidi na mashirika ya Korea Kusini. Mkutano wa Waziri huyo wa Uchumi wa Korea Kusini na Waziri wa Fedha wa Marekani ulifanyika Jumapili kando ya mkutano wa kiuchumi wa nchi wanachama wa kundi la G20 mjini Fukuyama, Japan.

Kim Dong-yeon, Waziri wa Uchumi wa Korea Kusini

Korea Kusini ni moja ya nchi nane ambazo baada ya Marekani kurejesha vikwazo vyake dhidi ya taifa la Iran, ilisamehewa na Rais Donald Trump katika uwanja wa vikwazo vya mafuta. Itakumbukwa kuwa mwaka jana na baada ya rais wa Marekani kutangaza kuiondoa nchi yake katika Mapatano ya Nyuklia ya JCPOA, alitangaza kurejesha vikwazo vya nyuklia dhidi ya nchi hii, suala ambalo lilipingwa vikali na nchi nyuklia za dunia.