Larijani: Iran haitakaa kimya mbele ya harakati za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54494-larijani_iran_haitakaa_kimya_mbele_ya_harakati_za_marekani
Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu nchini Iran (Bunge) amezungumzia hatua zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Tehran na kusema Jamhuri ya Kiislamu haitakaa kama mtazamaji tu mbele ya hatua hizo za Marekani.
(last modified 2026-09-18T11:23:09+00:00 )
Jul 01, 2019 22:30 UTC
  • Larijani: Iran haitakaa kimya mbele ya harakati za Marekani

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu nchini Iran (Bunge) amezungumzia hatua zinazochukuliwa na Marekani dhidi ya Tehran na kusema Jamhuri ya Kiislamu haitakaa kama mtazamaji tu mbele ya hatua hizo za Marekani.

Dakta Ali Lariijani ameashiria mienendo isiyo sawa na Rais Donald Trump wa Marekani dhidi ya watu wa Ulaya na China na kusema: Kiumbe muovu na mwenye madhara anayetawala Marekani anavuruga dunia kila siku kwa namna moja au nyingine. 

Spika wa Bunge la Iran amesema kuwa Donald Trump ana mienendo mibovu na ni mtu asiye na hadhi wala heshima katika upeo wa kimataifa. Ameongeza kuwa, ugaidi wa kiuchumi wa Trump dhidi ya Iran hautafanikiwa. 

Donald Trump

Dakta Larijani amesisitiza kuwa, kusimama kidete ndiyo njia pekee ya kukabiliana na mashinikizo ya Marekani na kuongeza kwamba: Kusimama kidete katika hali ya sasa ya Iran kuna maana ya kustawisha zaidi uzalishaji wa ndani. 

Tarehe 8 Mei mwaka jana wa 2018 Rais Doland Trump wa Marekani alioondoa nchi hiyo katika makubaliano ya kimataifa ya nyuklia kwa kifupi JCPOA na kuanza kuiwekea tena Iran vikwazo vya pande zote. 

Hatua hiyo ya Marekani ambayo ilikiuka sheria za kimataifa imelaaniwa na jamii ya kimataifa.