Video ya makomando wa SEPAH walipoisimamisha meli ya Uingereza Ghuba ya Uajemi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i54898-video_ya_makomando_wa_sepah_walipoisimamisha_meli_ya_uingereza_ghuba_ya_uajemi
Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesema kuwa halina muhali katika kutekeleza sheria na kulinda mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Jul 21, 2019 02:47 UTC

Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH limesema kuwa halina muhali katika kutekeleza sheria na kulinda mipaka ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Msemaji wa SEPAH, Ramadhan Sharif amesema kuwa, kikosi maalumu cha Jeshi la Majini la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (SEPAH) kimeisimamisha meli ya mafuta ya Uingereza ya "Stena Impero" baada ya meli hiyo kujaribu kupita kwenye Lango Bahari la Hormuz bila ya kuheshimu sheria za kimataifa ikiwa ni pamoja na kuzima kifaa chake cha GPS cha kuonesha eneo ilipo meli hiyo, kudharau maonyo yaliyotolewa na maafisa wa Iran, kupita katika njia siyo, kuendelea na safari yake licha ya kugonga boti ya uvuvi ya Iran, kuharibu mazingira kwa kuvujisha mafuta baharini n.k.

Meli hiyo ilikuwa inasindikwa na meli nyingine ya kivita ya Uingereza na ilijaribu kukizuia kikosi maalumu cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH kuisimamisha meli hiyo ya mafuta lakini ilishindwa.

Video iliyoambatana na habari hii ni ya kwanza kutolewa baada ya kusimamishwa meli hiyo ya mafuta ya Uingereza na Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH katika eneo la Ghuba ya Uajemi.