Kikao cha kamisheni ya pamoja ya JCPOA chaanza kufanyika Vienna, Austria
(last modified Sun, 28 Jul 2019 12:23:24 GMT )
Jul 28, 2019 12:23 UTC
  • Kikao cha kamisheni ya pamoja ya JCPOA chaanza kufanyika Vienna, Austria

Kikao cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia JCPOA cha Manaibu Mawaziri na Wakurugenzi wa Kisiasa wa Iran na kundi la 4+1 pamoja na mwakilishi wa Umoja wa Ulaya kimeanza leo huko Vienna mji mkuu wa Austria.

Abbas Araqchi, Naibu Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran na Helga Maria Schmid, Naibu Mkuu wa Sera za Kuigeni za Umoja wa Ulaya wanashiriki katika kikao kilichoanza leo cha kamisheni ya pamoja ya makubaliano ya nyuklia yanayojulikana kama Mpango Kamiili wa Pamoja wa Utekelezaji JCPOA kwa kifupi.

Kabla ya hapo Umoja wa Ulaya ulikuwa umetangaza kuwa, kikao hicho kinafanyika kwa ombi la Ufaransa, Ujerumani, Uingereza na Iran na kwamba, mambo mbalimbali yanayohusiana na makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yanatarajiwa kujadiliiwa.

Kikao cha Kkamisheni ya Pamoja yay JCPOA

Kabla ya kuanza kwa kikao hicho, kulifanyika mikutano ya pande mbili na pande kadhaa baina ya wajumbe wa kamisheni hiyo ya pamoja ya makubaliano ya JCPOA.

Aidha kikao hicho kinafanyika katika hali ambayo, hivi karibuni Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Mohammad Javad Zarif alisema kuwa, endapo madola ya Ulaya yatachukua hatua za lazima kwa ajili ya kutekeleza ahadi na wajibu wao kwa mujibu wa makubaliano ya JCPOA, basi Tehran inaweza kuangalia upya hatua ilizozichukua, vinginevyo Iran itaendelea kupunguza uwajibikaji wake kwenye mapatano hayo kwa mujibu wa kifungo cha 36 cha JCPOA. 

Tags