Rais Rouhani: Taifa la Iran halitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani
(last modified Fri, 02 Aug 2019 08:08:52 GMT )
Aug 02, 2019 08:08 UTC
  • Rais Rouhani: Taifa la Iran halitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya Marekani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, taifa hili katu halitasalimu amri mbele ya mashinikizo ya serikali ya Marekani.

Rais Rouhani amesema hayo katika kikao cha Baraza la Uongozi la Mkoa wa Azerbaijan Mashariki huko Tabriz kaskazini magharibi mwa Iran na kueleza kwamba, walimwengu wamefikia natija hii kwamba, taifa la Iran ni kubwa zaidi na lenye azma na irada zaidi kiasi kwamba, haliwezi kusalimu amri kwa mashinikizo kama ya Marekani.

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria kujitoa kinyume cha sheria Marekani katika makubaliano ya nyuklia ya Mapango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) na kuongezeka vikwazo dhidi ya Iran na kusema kwamba, kama makubaliano ya JCPOA yatabakia hadi mwaka ujao, vikwazo vyote vya sialaha vya Umoja wa Mataifa dhidi ya taifa hili vitaondolewa kikamilifu.

Iran imesimama kidete kukabiliana na njama na vikwazo vya Marekani dhidi yake

Rais Rouhani amebainisha kwamba, kisiasa na katika uga wa haki, makubaliano ya nyuklia ya JCPOA yana umuhimu mno kwa Iran, kwani ni kwa kupitia makubaliano hayo ya kimataifa ndipo Umoja wa Mataifa umetambua rasmi urutubishaji madini ya urani wa taifa hili.

Aidha amesema kuwa, wale ambao wanaipinga Iran hususan Wazayuni, utawala wa Saudi Arabia na Wamarekani wenye misimamo mikali, wameshindwa kuyastahamili makubaliano ya JCPOA na sasa wanatangaza wazi upinzani wao dhidi ya makubaliano haya ya kimataifa na wanakiri bayana kwamba, makubaliano haya yana manufaa kwa Iran mia kwa mia.

Tags