Iran ya Kiislamu yasali Swala ya Idul Adh'ha
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i55326-iran_ya_kiislamu_yasali_swala_ya_idul_adh'ha
Swala ya idul Adh'ha imefanyika leo asubuhi kwa kuhudhuriwa na wananchi wengi katika Iran nzima ya Kiislamu.
(last modified 2026-09-03T12:21:49+00:00 )
Aug 12, 2019 00:15 UTC
  • Iran ya Kiislamu yasali Swala ya Idul Adh'ha

Swala ya idul Adh'ha imefanyika leo asubuhi kwa kuhudhuriwa na wananchi wengi katika Iran nzima ya Kiislamu.

Sambamba na katika miji mingine ya Iran, swala ya Idul Haj imefanyika hapa Tehran katika uwanja wa sala wa Imam Khomeini chini ya Imamu Hujjatul Islam wal Muslimin Sayyid Muhammad Hassan Abuturabi Fard. Leo Jumatatu tarehe kumi Dhul-Hija mwaka 1440 Hijria ni Sikukuu ya Idul Adh'ha ambayo ni moja ya Sikukuu kubwa za Kiislamu. Mwenyezi Mungu aliijaribu imani na ikhlasi ya Nabii huyo kwa kumwamuru amchinje mwanawe kipenzi Ismail (as). Licha ya mashaka ya utekelezwaji wa amri hiyo, Nabii Ibrahimu (as) aliandaa mazingira ya kutekeleza amri hiyo na kumlaza chini mwanaye na kuanza kuikata shingo yake lakini kisu kilikataa kuchinja. Hapo ndipo alipoambiwa na Mwenyezi Mungu kuwa amefaulu mtihani huo na akamtumia mnyama wa kuchinja badala ya mwanaye Ismail. 

Hujjatul Islam Wal Muslimin Abuturabi Fard akiswalisha Sala ya Idul- Haj mjini Tehran
 

Tukio hili lenye ibra na mafunzo tele linawapa wanadamu somo la kujitoa mhanga, kujisabilia kwa ajili ya Allah, kushinda matamanio na matakwa ya nafsi na kusalimu amri mbele ya amri za Mwenyezi Mungu Mtukufu; na ndio maana Waislamu ulimwengu pia husherehekea tarehe kumi Dhul-Hija kama Sikukuu kubwa na yenye utukufu ya Kiislamu na kupata somo la dhati. 

Katika siku hii mahujaji wa Nyumba Tukufu ya Mwenyezi Mungu waliokwenda Makka, huchinja mnyama kwa ajili ya kutekeleza amri ya Mola wao na kuhuisha kumbukumbu ya Nabii Mtukufu Ibrahim (as).