Jan 12, 2020 12:05 UTC
  • Amir wa Qatar safarini Iran

Amir wa Qatar leo amewasili Tehran kwa lengo la kufanya mazungumzo an viongozi wa ngazi za juu wa Iran.

Tamim bin Hammad Al Thani, Amiri wa Qatar amewasili Tehran leo alasiri na kulakiwa na Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wiki iliyopita pia Waziri wa Mambo ya Nje wa Qatar  Sheikh Mohammed bin Abdulrahman Al Thani alitemebelea Iran na kufanya mazungumzo na rais wa Iran. 

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Qatar, mazungumzo ya viongozi wa nchi mbili yatagusia uhusiano baina ya nchi mbili na namna ya kuimarisha uhusiano huo. Aidha viongozi wa Iran na Qatar watajadili matukio ya hivi karibuni kieneo na kimetaifa.

 

Tags