Iran imeuza nje ya nchi bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 32
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imefanikiwa kuuza nje ya nchi bidhaa zenye thamani ya dola bilioni 32 katika kipindi cha mwaka huu wa Hijria Shamsia ambao unatazamiwa kumalizika Machi 21 2020.
Hatua hiyo imeweza kuimarisha uchumi wa nchi hii ambayo iko chini ya vikwazo vikali zaidi ambavyo havijawahi kushuhudiwa vya Marekani.
Naibu Waziri wa Viwanda wa Iran Hossein Modares Khiabani amesema mafanikio hayo ni sawa na muujiza kwa kuzingatia hali ya hivi sasa ya kiuchumi nchini.
Uchumi wa Iran umeanza kuimarika hatua kwa hatua baada ya msukosuko uliosababishwa na vikwazo vikali vya utawala wa Trump ambavyo vilianza Novemba 2018 wakati ambao Washington iliahidi kuwa itahakikisha uuzaji mafuta ghafi ya petroli ya Iran unafikia sifuri katika soko la kimataifa.
Vikwazo hivyo ni katika sera za Marekani za 'mashinikizo ya juu zaidi' dhidi ya Iran kwa lengo la kuilazimisha isalimu amri na kukubali mazungumzo mapya ya nyuklia sambamba na kufuta mpango wake wa makombora ya kujihami na kusitisha ushawishi wake katika eneo la Asia Magharibi.
Hata hivyo Iran imesisitiza kuwa haitalegeza msimamo wala kufanya mazungumzo mapya kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA yaliyofikiwa mwaka 2015 na ambayo Trump alitangaza kujiondoa Mei 2018.
Modares Khiabani amesema hivi sasa uuzaji nje ya nchi bidhaa zisizo za mafuta umechukua sehemu ya uuzaji wa
mafuta katika masoko ya kimataifa