Rouhani: Iran inafuatilia kwa karibu sana nyendo za Marekani
(last modified Sat, 25 Apr 2020 10:35:30 GMT )
Apr 25, 2020 10:35 UTC
  • Rouhani: Iran inafuatilia kwa karibu sana nyendo za Marekani

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Iran inafuatilia kwa karibu sana nyendo za Marekani na kuongeza kuwa: "Iran katu haitakuwa muanzishaji wa taharuki na mapigano katika eneo."

Rais Hassan Rouhani ameyasema hayo leo katika mazungumzo ya simu na Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Aal Thani ambapo sambamba na kuwasilisha salamu za kheri na fanaka kwa mnasaba wa kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa serikali na taifa la Qatar na pia kwa Waislamu kote duniani, ameelezea matumaini kuwa, mwezi huu utakuwa ni wenye baraka na kheri tele kwa umma wa Kiislamu.

Katika mazungumzo hayo ya simu, Amiri wa Qatar pia naye amewasilisha salamu za kheri na fanaka kwa serikali na taifa la Iran kwa mnasaba wa kuwadia Mwezi Mtukufu wa Ramadhani. Amiri wa Qatar amesema kuna udharura kwa nchi zote za eneo kufanya kila ziwezalo kuzuia taharuki.

Amiri wa Qatar Sheikh Tamim bin Aal Thani

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Amiri wa Qatar wamesema uhusiano wa Tehran na Doha ni chanya na unazidi kuimarika na wamesisitiza kuhusu udharura wa kuimarisha uhusiano wa pande mbili katika nyanja zote.

Tags