Mousavi: Hivi karibuni Marekani itapiga magoti mbele ya taifa la Iran
-
Sayyid Abbas Mousavi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amejibu msimamo wa maafisa wa Marekani kuhusiana na matokeo ya vikwazo vya nchi hiyo dhidi ya taifa la Iran na kusema: Karibini hivi Marekani itapiga magoti mbele ya taifa la Iran.
Sayyid Abbas Mousavi ameyasema hayo baada ya Mwakilishi Maalumu wa Marekani katika Masuala ya Iran, Brian Hook kuviambia vyombo vya habari kwamba, Washington imeridhishwa na matokeo ya vikwazo vyake dhidi ya Iran.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Irani amekemea ugaidi wa kiuchumi wa Merekani kwa watu wa Irani, akisema sera za vikwazo za Washington zimefeli na kwamba utawala huo hivi karibuni utapiga magoti mbele ya Taifa la Irani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran ameandika leo Ijumaa katika ukurasa wake wa Twitter kwamba: "Serikali ambayo sera zake zimejengeka juu ya siasa za kushindilia kwa goti shingo za watu wake yenyewe na watu wa mataifa mengine inapaswa kufurahia ugaidi na mashinikizo dhidi ya raia wa kawaida."
Mousavi alikuwa akiashiria mauaji ya kikatili ya rais mwenye asili ya Afrika wa Marekani, George Floyd, ambaye alipoteza maisha baada ya polisi mweupe kubinya shingo yake kwa goti kwa karibu dakika tisa huko Minneapolis, Mei 25.
Mousavi ameongeza kuwa: "Maafisa wa Marekani wameelewa kwamba kwa ugaidi wao wa kiuchumi hawakuvunja shingo ya taifa la Iran, bali wamevunja magoti yao wenyewe na karibuni watapiga magoti mbele ya taifa la Iran."