Watu zaidi ya 155,000 walioambukizwa COVID-19 nchini Iran wapona
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i61658-watu_zaidi_ya_155_000_walioambukizwa_covid_19_nchini_iran_wapona
Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran ametangaza kuwa, hadi hivi sasa waathirika 155,00 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona nchini Iran wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 17, 2020 06:20 UTC
  • Watu zaidi ya 155,000 walioambukizwa COVID-19 nchini Iran wapona

Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran ametangaza kuwa, hadi hivi sasa waathirika 155,00 wa ugonjwa wa COVID-19 au corona nchini Iran wamepona na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini.

Bi. Sima Sadat Lari Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran ametangaza hayo leo Jumatano katika kikao cha kila siku na waandishi habari na kuongeza kuwa wagonjwa wapya 2,612 wa COVID-19 wamegundulika Iran katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kufikia leo adhuhuri.

Bi. Sadat Lari amesema baina ya kesi mpya za maambukizi zilizoripotiwa, 1,071 wamelazwa hospitaliani na waliosalia wamepata matibabu bila kulazwa na kwamba kwa ujumla watu walioambukizwa COVID-19 nchini Iran ni 195,051.

Hali kadhalika ameashiria kufariki dunia wagonjwa 120 wa corona nchini Iran katika kipindi cha masaa 24 hadi kufikia leo adhuhuri na kusema kuwa, hadi sasa watu 9,185 wameaga dunia kwa COVID-19 hapa nchini.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran hadi sasa nchini Iran kumefanyika vipimo milioni 1 na 320 elfu vya COVID-19.

Idadi jumla ya walioambukizwa COVID-19 duniani hadi kufikia Alhamisi ilikuwa takribani milioni 7.94 na waliopoteza maisha ni zaidi ya 535,000.

Marekani inaongoza duniani kwa maambukizi na vifo vya corona ambapo hadi kufikia leo watu zaidi ya milioni 2.8 walikuwa wameambukizwa COVID-19 na wengine wasiopungua 119,000 wamepoteza maisha.