COVID-19 nchini Iran: zaidi ya watu 215,000 wapata afueni
Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran ametangaza kuwa, hadi hivi sasa waathirika laki mbili na 15 elfu ugonjwa wa COVID-19 au corona humu nchini wamepata afueni na kuruhusiwa kurejea nyumbani kutoka mahospitalini na katika vituo vya afya.
Bi. Sima Sadat Lari, Msemaji wa Wizara ya Afya ya Iran ametangaza hayoIjumaa na kuongeza kuwa, wagonjwa wapya takribani 2000 wa COVID-19 wamegunduliwa nchini Iran katika kipindi cha masaa 24 yaliyopita kufikia jana adhuhuri. Amesema miongoni mwa kesi hizo mpya, wagonjwa 455 wamelazwa hospitalini na waliosaliwa wamepatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani.
Bi. Sadat Lari amongeza kuwa kwa ujumla watu walioambukizwa COVID-19 nchini Iran hadi jana mchana walikuwa 252,720. Halikadhalika aliongeza kuwa katika kipindi cha masaa 24 hadi jana adhuhuri, watu 142 walipoteza maisha kutokana na COVID-19 na hivyo kufanya idadi ya waliopoteza maisha Iran kutokana na ugonjwa huo kufika 12,447.
Idadi jumla ya walioambukizwa COVID-19 duniani hadi kufikia Ijumaa jioniilikuwa takriban milioni 12.3 na na waliopoteza maisha hadi leo mchana ilikuwa ni zaidi ya watu zaidi ya 555,000 .
Marekani inaongoza duniani kwa maambukizi na vifo vya COVID-19 ambapo hadi kufikia Ijumaa jioni watu zaidi ya 3,165,058 walikuwa wameambukizwa COVID-19 na wengine wasiopungua 135,094 walikuwa wamepoteza maisha nchini Marekani pekee.