Rouhani: Adui hajaweza kuizuia Iran kuuza bidhaa nje ya nchi
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62487-rouhani_adui_hajaweza_kuizuia_iran_kuuza_bidhaa_nje_ya_nchi
Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema adui hajaweza kuizuia Iran kuuza bidhaa zake nje ya nchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 29, 2020 03:15 UTC
  • Rouhani: Adui hajaweza kuizuia Iran kuuza bidhaa nje ya nchi

Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema adui hajaweza kuizuia Iran kuuza bidhaa zake nje ya nchi.

Akizungumza katika kikao cha baraza la mawaziri leo asubuhi mjini Tehran, Rais Rouhani amesema: "Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita na hasa miezi michahce iliyopita, Iran imepitia kipindi kigumu lakini pamoja na hayo nchi imeweza kukidhi mahitaji ya kimsingi ya wananchi."

Rais Rouhani amesema Iran sasa imezidi kuimarika mbele ya njama zote za maadui na wasioitakia mema nchi hii. Ameongeza kuwa mpango wa kwanza wa maadui ulikuwa ni kuuvuruga uchumi wa Iran na kuwaweka wananchi chini ya mashinikizo ya kiuchumi lakini sasa, kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu, Iran imesambaratisha njama za maadui na msingi wa nchi na mfumo uko imara.

Rais Rouhani amesema sekta ya viwanda na uzalishaji nchini imefanya kazi nzuri kwani  leo taifa la Iran mbali na kuwa linajizalishia bidhaa za kutumia ndani ya nchi pia imeweza kuimarisha uuzaji nje ya nchi bidhaa zisizo za mafuta.

Bandari ya Chabahar kusini mwa Iran

Aidha amesema baada ya mkataba wa Iran na Muungano wa Kiuchumi wa Eurasia kuanza kutekelezwa mwishoni mwa mwezi Juni, mauzo ya Iran katika nchi za Eurasia yaliongezeka kwa asilimia 63. Amesema pamoja na kuwepo janga la corona, Iran imewezea kuongeza kiwango cha bidhaa zake zinazouzwa nje ya nchi.

Hali kadhalika Rais Rouhani ameashiria njama za hivi karibuni za maadui dhidi ya Iran na kusema: "Mojawapo ya mbinu za maadui ni kuibua mifarakano ndani ya nchi. Mapema mwaka huu wakati wa mwanzo wa janga la corona, maadui walijaribu kuibua hitilafu baina ya mihimili ya dola lakini tulifanikiwa kusambaratisha njama hiyo.