Iran: Baraza la Ghuba ya Uajemi liache kutii Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62757-iran_baraza_la_ghuba_ya_uajemi_liache_kutii_marekani
Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwepo wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi ni kinyume cha sheria na chanzo cha ukosefu wa usalama na uthabiti na hivyo nchi wananchama za Baraza la Uhusiano la Ghuba ya Uajemi hazipaswi kuitii Marekani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 11, 2020 23:19 UTC
  • Iran: Baraza la Ghuba ya Uajemi liache kutii Marekani

Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema uwepo wa Marekani katika eneo la Ghuba ya Uajemi ni kinyume cha sheria na chanzo cha ukosefu wa usalama na uthabiti na hivyo nchi wananchama za Baraza la Uhusiano la Ghuba ya Uajemi hazipaswi kuitii Marekani.

Mahmoud Vaezi amezungumzia suala hilo kupitia ukurasa wake wa Twitter kufuatia barua ya Katibu Mkuu wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ambaye ametaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lirefushe vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.

Mkuu wa Ofisi ya Rais wa Iran amesema: "Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa halipaswi kuifuata Marekani, ambayo uwepo wake katika eneo haujaleta chochote isipokuwa ukosefu wa usalama na uthabiti.

Katibu Mkuu wa Barazala la Ushirikino la Ghuba ya Uajemi, Nayef Fallah Mubarak Al-Hajraf siku ya Jumamosi, ikiwa ni katika kufuata sera hasimu za Marekani dhidi ya Iran, aliliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa akitaka kuongezwa muhula wa vikwazo vya silaha dhidi ya Iran.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

Marekani imeanzisha kampeni kubwa za kimataifa za kulizuia Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa litekeleze azimio lake nambari 2231 linalotoa amri ya kuiondolea Iran vikwazo vya silaha ifikapo tarehe 18 Oktoba mwaka huu wa 2020. Marekani inaendesha njama hizo kama sehemu ya kukabiliana na uwezo mkubwa wa kiulinzi na kijeshi wa Iran unaozidi kukua na kuwa imara siku baada ya siku