Iran yaitaka dunia isimame na kupinga uvunjaji sheria wa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62762-iran_yaitaka_dunia_isimame_na_kupinga_uvunjaji_sheria_wa_marekani
Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mataifa ya dunia yanapaswa kusimama na kupinga hatua za Marekani za kukanyaga na kukiuka sheria za kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 12, 2020 03:30 UTC
  • Iran yaitaka dunia isimame na kupinga uvunjaji sheria wa Marekani

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, mataifa ya dunia yanapaswa kusimama na kupinga hatua za Marekani za kukanyaga na kukiuka sheria za kimataifa.

Dakta Muhammad Javad Zarif amesisitiza kwamba, walimwengu hawapaswi kufumbia macho na kunyamazia kimya uvunjaji sheria unaofanywa na serikali ya Marekani.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameongeza kuwa, kile ambacho tumekishuhudia kutoka kwa serikali ya sasa ya Marekani ni kwamba, haina mipango yoyote ile ya maana na inayoeleweka kwa ajili ya mustakabali wa jamii ya kimataifa.

Kadhalika Dakta Zarif ameeleza kuwa, tunaona hata jinsi serikali ya sasa ya Marekani ilivyoshindwa kukabiliana na janga la virusi vya corona kutokana na mipango yake mibovu.

Rais Donald Trump wa Marekani ambaye serikali yake imekuwa ikijitoa katika mikataba ya kimataifa 

Kuhusiana na sera za kigeni za Marekani, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa, Washington haina mipango ya kweli isipokuwa kufanya hujuma tena kwa upofu dhidi ya kila anayeheshimu na kuunga mkono sheria.

Dakta Zarif amebainisha kwamba, mfano wa wazi wa ukiukaji wa wazi wa sheria na mikataba ya kimataifa unaofanywa na Marekani ni hatua ya serikali ya Trump ya kukiuka azimio nambari 2231 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lililounga na kuidhinisha makubaliano ya nyuklia yaliyofikkiwa baina ya Iran na kundi la 5+1 ikiwemo Marekani yenyewe.