Naibu Kamanda wa SEPAH azionya Imarati na utawala haramu wa Israel
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i62970-naibu_kamanda_wa_sepah_azionya_imarati_na_utawala_haramu_wa_israel
Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH amezionya Imarati na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, Iran itatoa jibu kali kwa chokochoko yoyote ile.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 22, 2020 19:33 UTC
  • Naibu Kamanda wa SEPAH azionya Imarati na utawala haramu wa Israel

Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH amezionya Imarati na utawala haramu wa Israel na kusisitiza kwamba, Iran itatoa jibu kali kwa chokochoko yoyote ile.

Jenerali Ali Fadavi amesema hayo katika mahojiano aliyofanyiwa na Shirika la Habari la Iran Press ambapo amesisisitiza kwamba, endapo Imarati na Israel zitafanya harakati japo ndogo yenye kutishia usalama wa taifa hili, basi Iran itatoa jibu kali kwa hatua hiyo. 

Naibu Kamanda Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu  ya Iran SEPAH ameongeza kuwa, uwanja huu mpya uliofunguliwa na Wazayuni na Wamarekani, utashindwa ilivyokuwa huko nyuma na ushindi utakuwa ni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Imarati na Israel hivi karibuni zilitangaza kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia baina yao huku kukiwa na tetesi kwamba, Saudi Arabia nayo iko njiani kufuata mkondo huo

Kamanda huyo mwandamizi wa Jeshi la Walinzi wa Mpainduzi ya Kiislamu SEPAH ameashiria pia njama za maadui za kutaka kutoa pigo dhidi ya Iran ya Kiislamu na kusema kuwa, uwezo na nguvu za Iran ni kubwa mno ikilinganishwa na miaka 41 iliyopita kiasi kwamba, zinamfanya adui asithubutu kuanzisha chokochoko dhidi ya taifa hili.

Kufuatia hatua kadhaa zilizochukuliwa na Rais Donald Trump wa Marekani kwa lengo la kurahisisha uanzishwaji wa uhusiano wa kawaida kati ya Imarati na utawala haramu wa Kizayuni, Alkhamisi iliyopita ya tarehe 13 Agosti pande mbili za Abu Dhabi na Tel Aviv zilisaini mkataba na kuafikiana rasmi kuanzisha uhusiano kamili wa kidiplomasia.  Hatua hiyo imeendelea kulaaniwa na watu huru na wapigania uadilifu kote ulimwenguni.