Takribani wagonjwa 334,000 wa COVID-19 nchini Iran wamepata afueni
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63257-takribani_wagonjwa_334_000_wa_covid_19_nchini_iran_wamepata_afueni
Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, wagonjwa waliopata afueni ya ugonjwa ya ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini imefikia takribani watu 334,000.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 06, 2020 06:54 UTC
  • Takribani wagonjwa 334,000 wa COVID-19 nchini Iran wamepata afueni

Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran imetangaza kuwa, wagonjwa waliopata afueni ya ugonjwa ya ugonjwa wa Covid-19 hapa nchini imefikia takribani watu 334,000.

Sima Sadat Lari, msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran amesema hayo leo wakati akitoa takwimu mpya za watu waliokumbwa na virusi vya corona hapa nchini Iran na akabainisha kuwa: Kwa mujibu wa matokeo ya vipimo rasmi, katika muda wa saa 24 zilizopita wagonjwa wapya 1,992 waliokumbwa na ugonjwa wa Covid-19 wamegunduliwa hapa nchini, ambapo 902 miongoni mwao wamelazwa hospitali na waliosalia wamepatiwa huduma za tiba na kuruhusiwa kurudi nyumbani.

Bi Lari amefafanua kuwa, idadi ya watu waliougua ugonjwa wa Covid-19 nchini Iran imefikia 386,658 na kutokana na wagonjwa 139 kuaga dunia katika kipindi cha saa 24 zilizopita, jumla ya watu waliofariki dunia kutokana na ugonjwa huo hadi sasa hapa nchini imefikia 22,293.

Kwa mujibu wa msemaji wa Wizara ya Afya, Tiba na Mafunzo ya Utabibu ya Iran hadi kufikia leo mchana, wagonjwa 333,900 wamepata afueni na kuruhusiwa kutoka hospitalini na kurejea majumbani.

Huku hayo yakiripotiwa, idadi ya watu waliokumbwa na virusi vya corona duniani kote imepindukia 27,000,000. Miongoni mwa hao, watu zaidi ya 884,000 wameshaaga dunia na wengine wapatao 20,000,000 wamepata nafuu na kuruhusiwa kutoka hospitali.

Marekani imeendelea kuwa nchi iliyoathiriwa zaidi na virusi vya corona duniani, ikifuatiwa na Brazil, India, Russia na Peru.