Marajii Taqlidi walaani kuvunjiwa heshima Qur'an Tukufu na Mtume Muhammad SAW
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63259-marajii_taqlidi_walaani_kuvunjiwa_heshima_qur'an_tukufu_na_mtume_muhammad_saw
Marajii Taqlidi wa Waislamu wa Kishia wamelaani kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu huko nchini Sweden na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW huko nchini Ufaransa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 06, 2020 06:55 UTC
  • Marajii Taqlidi walaani kuvunjiwa heshima Qur'an Tukufu na Mtume Muhammad SAW

Marajii Taqlidi wa Waislamu wa Kishia wamelaani kitendo cha kuchomwa moto Qur'ani Tukufu huko nchini Sweden na kuvunjiwa heshima Mtume Muhammad SAW huko nchini Ufaransa.

Ayatullah Abdollah Javad-Amoli, Marjaa Taqlidi wa Qum Iran ametoa ujumbe na kulaani kitendo cha kuchomwa moto nakala ya Kitabu Kitakatifu cha Qur'ani huko nchini Sweden na kuvunjiwa heshima Bwana Mtume SAW na gazeti la Kifaransa la Charlie Hebdo na kuitahadharisha Ufaransa na mataifa mengine kwamba, yasiruhusu katika nchi zao mtu aivunje heshima Qur'ani au Mtume SAW, Mtume yeyote yule wa Mwenyezi Mwenyezi Mungu au kitabu chochote kile cha mbinguni.

Aidha kiongozi huyo wa kidini amesema kuwa, kama madola ajinabi yanakusudia kuzusha fitina na mifarakano baina ya mataifa ya dunia kupitia njia hii basi hayatafanikiwa katika njama yao hiyo.

Gazeti la Kifaransa la Cahrlie Hebdo ambalo limekuwa likichapisha mara kwa mara vikatuni vya kumvunjia heshima Bwana Mtume SAW

Kwa upande wake, Ayatullah Hossein Noori-Hamedani, Marjaa na kiongozi mwingine wa ngazi za juu wa kidini hapa nchini Iran amesema kuwa, kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu ni njama za vituo vya kifikra vya Wazayuni na Marekani zinazofanyika katika fremu ya kueneza chuki na hofu dhidi ya Uislamu.

Hivi karibuni, watu wenye chuki dhidi ya Uislamu walichoma moto na kuteketeza nakala ya Qur'ani katika mji wa Malmo nchini Sweden. Aidha wiki iliyopita, jarida la Charlie Hebdo la Ufaransa lilichapisha katuni na vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (S.A.W). Vitendo hivyo vya chuki dhidi ya Uislamu vimeendelea kulaaniwa kila kona ya Ulimwengu wa Kiislamu.