Hatami: Lengo la kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani ni kupunguza kudhalilishwa Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i63579-hatami_lengo_la_kuuliwa_kigaidi_luteni_jenerali_soleimani_ni_kupunguza_kudhalilishwa_marekani
Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, lengo la adui la kumuua kigaidi na kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni kupunguza kudhalilishwa zaidi Marekani katika eneo hili.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 22, 2020 08:39 UTC
  • Hatami: Lengo la kuuliwa kigaidi Luteni Jenerali Soleimani ni kupunguza kudhalilishwa Marekani

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa, lengo la adui la kumuua kigaidi na kidhulma Luteni Jenerali Qassem Soleimani, Mkuu wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH ni kupunguza kudhalilishwa zaidi Marekani katika eneo hili.

Shirika la habari la IRNA limeripoti habari hiyo na kumnukuu Brigedia Jenerali Amir Hatami akisema leo Jumanne katika sherehe maalumu zilizofanyika kwa njia ya video kwamba Luteni Jenerali Shahid Qassem Soleimani daima alikuwa akiziweka hai roho na nyoyo za wapigania ukombozi duniani. Ameongeza kuwa, nguvu na mori wa kulipiza kisasi damu ya kamanda huyo ziko vile vile na lazima wahusika wa jinai hiyo watalipa damu za shahid Soleimani na mashahidi wenzake.

Vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Iraq katika mapambano dhidi ya magenge ya kigaidi ya mabeberu

 

Waziri wa Ulinzi wa Iran vile vile amesema kuwa vita vya kujihami kutakatifu ambavyo taifa la Iran lililazimishwa kupigana vimelipa fakhari, nguvu na heshima taifa la Iran. Amesema, hali ya hivi sasa ya Iran ya Kiislamu katika nyuga tofauti za kielimu, kisiasa na hasa katika upande wa ulinzi ni kwa namna ambayo licha ya kuweko vitisho mbalimbali vya mfumo wa kibeberu lakini Iran ina uwezo wa kugundua tishio lolote katika eneo linakotokea hata nje ya mipaka ya ardhi yake.

Brigedia Jenerali Hatami pia amesema, ushahidi wa wazi na wa kivitendo wa nguvu hizo za Iran umeonekana katika nyakati tofauti na kutoa mfano kwa kusema, wakati adui ameingiza magenge ya kigaidi katika ardhi za nchi kubwa kwa ajili ya kuziteka, Iran ya Kiislamu imeonesha nguvu zake kwa kuzisaidia kiushauri nchi mbili za Kiarabu za Iraq na Syria na kufanikiwa kumshinda adui na magenge yake katili ya kupandikiza.