Marekani inachochea chuki dhidi ya Uislamu
(last modified Thu, 05 May 2016 08:36:30 GMT )
May 05, 2016 08:36 UTC
  • Marekani inachochea chuki dhidi ya Uislamu

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema Marekani inachochea chuki dhidi ya Uislamu, Iran na Ushia.

Ayatullah Seyyed Ali Khamenei Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo leo Alhamisi asubuhi mjini Tehran alipohutubu katika kikao kilichohudhuriwa na maafisa wa ngazi za juu wa mfumo wa Kiislamu, mabalozi wa nchi za Kiislamu hapa Tehran na wananchi wa matabaka mbali mbali kwa munasaba wa siku kuu ya kukumbuka kubaathiwa na kupewa Utume, Mtume Muhammad al Mustafa SAW.

Katika hotuba yake Kiongozi Muadhamu amesema hivi karibuni Wamarekani walitangaza kuwa sera za Iran katika eneo ni chanzo cha kuwekewa nchi hii vikwazo na kukabiliana nayo. Amesema Marekani inataka Iran irudi nyuma ili iweze kufanya kila inalotaka. Kiongozi Muadahmu amesema katu Iran haiwezi kulegeza misimamo yake kwani huo utakuwa ni ujahiliya.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema leo wanaadamu zaidi ya wakati wowote ule wanahitaji kufahamu maana na ukweli halisi wa kubaathiwa Mtume SAW. Amesema Idi ya Mabaath ni idi ya mwamko na kumuondolea mwanadamu masaibu.