Kinara wa propaganda za ghasia anyongwa Iran
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i65147-kinara_wa_propaganda_za_ghasia_anyongwa_iran
Ruhullah Zam, kinara wa mtandao wa habari wa Amad News ambao ulikuwa unaeneza propagadna dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu amenyongwa kufuatia hukumu iliyotoelwa na mahakama.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 12, 2020 03:37 UTC
  • Kinara wa propaganda za ghasia anyongwa Iran

Ruhullah Zam, kinara wa mtandao wa habari wa Amad News ambao ulikuwa unaeneza propagadna dhidi ya Mapinduzi ya Kiislamu amenyongwa kufuatia hukumu iliyotoelwa na mahakama.

Ruhullah Zam, kinara wa tovuti na mtandao wa habari wa Amad News, ambaye binafsi alijinadi kuwa kinara wa ghasia na mchafuko nchini Iran amenyongwa leo asubuhi kufuatia hukumu ya kifo iliyotolewa dhidi yake na mahakama.

Kwa miaka kadhaa, Zam alikuwa akitumiwa na mashirika ya kijasusi ya ajinabi pamoja na makundi ya wanaopinga Mapinduzi ya Kiislamu ambapo alisaidiwa kuanzisha mtandao wa habari wa Amad News nje ya Iran.

Mtandao huo wa habari ulikuwa ukieneza habari bandia na feki dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa lengo la kuvuruga usalama wa nchi.

Ruhullah Zam akiwa mahakamani wakati wa kusikilizwa kesi yake

Mamluki huyo alikamatwa katika oparesheni maalumu ya Idara ya Intelijensia ya Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kisha akafikishwa mahakamani ambapo alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifo kwa kutiwa kitanzi.

Mtandao wa Amad News ulikuwa ukieneza habari bandia kuhusu maafisa wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran sambamba na kuibua hali ya kukosa matumaini miongoni mwa wananchi. Mtandao huo wa habari bandia ulilenga kupotosha fikra za umma na kuimarisha irada ya maadui na mashirika ya kijasusi ya ajinabi ili kuuangusha mfumo wa Kiislamu wa Iran.