Dec 30, 2020 14:36 UTC
  • Rouhani: Taifa la Iran litaikata miguu Marekani katika eneo

Rais Hassan Rouhani amesema Jamhuri ya Kiislamu ya Iran itaikata miguu Marekani katika eneo la Asia Magharibi katika kisasi chake cha mauaji ya kigaidi ya Luteni Jenerali Qassem Suleimani, Kamanda wa zamani wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (SEPAH).

Rais Rouhani amesema hayo leo Jumatano katika kikao cha Baraza la Mawaziri na kuongezeka kuwa: Mlikata mikono ya Jenerali wetu na miguu yenu itakatwa katika eneo.

Dakta Rouhani ameeleza bayana kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ina haki ya kulipiza kisasi cha damu ya Shahidi Suleimani na kwamba "madhali mungalipo katika eneo, ina maana kwamba bado hatujalipiza kisasi cha mwisho."

Huku akiashiria kuwa Shahidi Suleimeni alikuwa shujaa wa taifa la Iran na fahari ya nchi zote za Kiislamu, Rais wa Iran amebainisha kuwa, mauaji ya Shahidi Suleimeni kilikuwa kisasi cha maadui dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, mataifa ya eneo hili la Asia Magharibi na uhuru wa kujitawala nchi za eneo. 

Ameongeza kuwa, "Kisasa hicho (cha maadui) kilikuwa dhidi ya mataifa shupavu ya eneo yaliyosimama kidete dhidi ya njama za maadui na Uzayuni. Hawakutana kuona mamluki wao wa Daesh (ISIS) wanasambaratishwa katika eneo namna walivyosambaratishwa."

Shahidi Suleimani

Dakta Rouhani amesema hakuna yeyote anayefaidika na ukosefu wa usalama katika nchi za Yemen, Syria, Iraq, Lebanon, na Afghanistan ghairi ya Wazayuni.

Jenerali Suleimani aliuawa shahidi alfajiri ya kuamkia Ijumaa ya tarehe 3 Januari 2020 pamoja na Abu Mahdi al Muhandis, aliyekuwa Naibu Mkuu wa Al-Hashdu-Sha'abi pamoja na wenzao wengine wanane katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad nchini Iraq.

Tags