Zarif: UN haina faili safi katika suala la kutetea sheria za kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i67184-zarif_un_haina_faili_safi_katika_suala_la_kutetea_sheria_za_kimataifa
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa hauna faili zuri katika kutetea sheria za kimataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 23, 2021 10:13 UTC
  • Muhammad Javad Zarif
    Muhammad Javad Zarif

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa, Umoja wa Mataifa hauna faili zuri katika kutetea sheria za kimataifa.

Muhammad Javad Zarif leo ameashiria suala la kushindwa Umoja wa Mataifa kutetea haki na sheria za taifa la Iran katika vita vya kulazimishwa vilivyoanishwa na utawaka wa Saddam Hussein dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu na kueleza kuwa: Umoja wa Mataifa hauna faili safi katika suala la kutetea haki za kimataifa.  

Akizungumza katika Kongamano la Kimataifa  la Kupigania Sheria za Kimataifa, Zarif ameongeza kuwa, kazi ya taasisi za kimataifa si kubadili nguvu, bali ni kurekebisha matumizi ya nguvu kama wenzo na kuyafany kuwa ya kisheria.

Zarif ameeleza kuwa, Umoja wa Mataifa haukutumia hata wenzo huo wa kurekebisha matumizi ya nguvu wakati wa vita vya kulazimishwa vya Saddam Hussein dhidi ya Iran. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema, shambulio lililofanywa na utawala wa Baath wa dikteta wa zamani wa Iraq dhidi ya Iran ni ukikaji wa sheria za kimataifa na kueleza kuwa: Shambulio hilo la kijeshi lilitekelezwa kwa lengo la kujitanua na linahesabiwa kuwa ni uvamizi kwa mujibu wa sheria na kanuni zote. Zarif amesisitiza kuwa, ripoti za Umoja wa Mataifa zinaonyesha kuwa utawala wa Baath wa Iraq ulitekeleza hatua zilizokusudiwa kwa malengo maalumu ili kuharibu maeneo ya raia.  

Dikteta wa zamani wa Iraq, Saddam Hussein 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ameashiria mashambulizi ya utawala wa Baath wa Iraq katika miji mbalimbali ya Iran na kueleza kuwa: Kile kilichojukuja kujulikana kama "vita vya miji" ni jinai ya kivita. 

Kongamano la Kimataifa la Kupigania Sheria za Kimataifa limeanza leo katika Jumba la Makumbusho la Mapinduzi ya Kiislamu na Kujitetea Kutakatifu mjini Tehran.