Jun 15, 2021 07:26 UTC
  • Kiongozi wa Ahul Sunna: Kushiriki kwa wingi katika uchaguzi wa rais wa Iran kutavunja njama za adui

Mwanachama wa Baraza la Fatwa la Ahul Sunna Kusini mwa Iran amesema kushiriki kwa wingi wananchi katika uchaguzi ujao wa Ijumaa nchini Iran kutavunja njama za maadui.

Sheikh Mohammad Ali Amini, mwanachama wa Baraza la Fatwa la Ahul Sunna Kusini mwa Iran ameyasema hayo Jumanne katika mahojiano na IRNA na kuongeza kuwa, wasomi katika jamii, viongozi wa kikabila na watu wenye ushawishi katika jamii wanawajibika kuwashawishi wananchi kushiriki katika uchaguzi sambamba na kuarifisha mgombea bora.

Sheikh Mohammad Ali Amini ameongeza kuwa, uchaguzi ni haki ya kikatiba na wajibu wa wananchi wote waliotimiza masharti kutumia haki yao ya kupiga kura.

Mwanachama wa Baraza la Fatwa la Ahul Sunna Kusini mwa Iran  aidha amesema vyombo vya habari ndani ya nchi vinapaswa kusambaratisha njama chafu za maadui ili wananchi waweze kushiriki kwa wingi katika uchaguzi.

Wagombea urais katika uchaguzi wa rais Iran mwaka 2021

Uchaguzi wa 13 wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran unatarajiwa kufanyika Ijumaa ya wiki ijayo ya tarehe 18 mwezi huu wa Juni, 2021 ndani na nje ya nchi. Wagombea urais katika uchaguzi huo ni Saeed Jalili, Mohsen Rezaee Mirgha'ed, Sayyid Ebrahim Raisi, Alireza Zakani, Sayyid Amir-Hossein Ghazizadeh Hashemi, Mohsen Mehralizadeh na Abdolnaser Hemmati.

Rais wa sasa Hassan Rouhani anayemaliza muhula wake wa pili mfululizo haruhusiwi kugombea urais katika awamu hii.

Wagombea hao wa Urais wanaendelea kunadi sera zao katika majukwaa mbalimbali, na tayari wameshashiriki katika mdahalo wa tatu na wa mwisho wa urais.

Tags