Kuondolewa Iran vizingiti vya benki, mada kuu ya kikao cha London
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i7531-kuondolewa_iran_vizingiti_vya_benki_mada_kuu_ya_kikao_cha_london
Vikwazo vya kinyuklia dhidi ya Iran viliondolewa miezi kadhaa iliyopita baada ya kuanza kutekelelzwa mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 21, 2016 23:51 UTC
  • Kuondolewa Iran vizingiti vya benki, mada kuu ya kikao cha London

Vikwazo vya kinyuklia dhidi ya Iran viliondolewa miezi kadhaa iliyopita baada ya kuanza kutekelelzwa mapatano ya nyuklia yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).

Katika kipindi chote hicho, idadi kubwa ya wanasiasa na wanaharakati wa kiuchumi wamefika Iran kwa ajili ya kujitayarisha kuanzisha harakati mpya za kibiasahra na kiuchumi nchini.

Pamoja na hayo, ripoti zinaonyesha kuwa, bado kuna vizingiti katika miamala ya kibiashara na kiuchumi baina ya Iran na nchi nyingine. Moja ya vizingiti hiyo ni kuendelea kuzuiwa Iran kujiunga kikamilifu na mfumo wa benki duniani.

Marekani na washirika wake barani Ulaya akiwemo mkuu wa sera za kigeni katika Umoja huo, Bi Federica Mogherini walikutana Alkhamisi mjini London kujadili kadhia hiyo.

Katika kikao hichi benki za Ulaya zimetakiwa kuwekeza nchini Iran. Aidha walisistiza kuwa hivi sasa sehemu kubwa ya vikwazo vimeondolewa ili kuhimiza biashara ya kisheria na Iran.

Baada ya kikao hicho, wakuu wa Ulaya waliahidi kusaidia na kuhimiza mashirika ya bara hilo kuanzisha uhusiano wa kibiashara na Iran.

Katika taarifa ya pamoja nchi hizo zilisema: "Sisi hatuzuia shughuli za biashara halali na Iran. Sisis hatuzuii mashirika ya kifedha au mashirika ya kimataifa kufanya kazi na Iran. Idhini hii ipo maadamu taasisi na mashirika yote yanazingatia sheria zilizopo."

Kwa upande wake, Valiollah Seif, Mkuu wa Benki Kuu ya Iran ambayo pia alishiriki katika kikao hicho cha London kilichopewa jina la Euromoney Iran Conference, amezitaka nchi za Magharibi kutekeleza ahadi zao kivitendo. Siku ya Ijumaa, Seif alikutana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Philip Hammond ambapo alisisitiza kwa mara nyingine ulazima wa nchi za Magharibi kutekeleza ahadi zao kuhusu shughuli za kibenki kwa mujibu wa mapatano ya nyuklia.

Hammond pia katika kikao hicho alisisitiza kuwa Uingereza itatekeleza ahadi zake kwa mujibu wa mapatano ya nyuklia ya Iran. Aidha amesema serikali yake inazishawishi pia nchi zote za Ulaya zianzisha mfumo unaofaa wa kuwa na uhusiano wa kawaida wa kibenki na Iran.

Wiki kadhaa zilizopoita, mji wa London ulikuwa mwenyeji wa wakurugenzi wa benki kubwa za Ulaya ambapo washiriki walijadili njia za kurejesha uhusiano wa kawaida wa kibenki na Iran. Uzoefi unaonyesha kuwa, katika vikao hivyo hutolewa ahadi chungu nzima na kwa hivyo sasa kunahitajika hatua za kivitendo ili benki za Iran ziweze kuwa na uhusiano wa kawaida na benki nyingine za kimataifa.

Tokea mapatano ya nyuklia yaanze kutekelezwa, na mashirika mengi ya Ulaya yameonyosha nia ya kufanya biashara na Iran. Lakini idadi kubwa ya mashirika hayo yana wasiwasi kuhusu kuadhibiwa na Marekani kama yatafanya biashahra na Iran.

Kwa msingi huo Marekani ndiyo ambayo imekuwa ikivunja ahadi zake katika mapatano ya nyuklia na kuzitishia nchi nyingine zinazotaka kufanya biashara na Iran. Hii ni katika hali ambayo Iran imetekeleza kikamilifu ahadi zake zote kwa mujibu wa mapatano ya nyuklia.