Raisi: Kulinda mazingira ni jambo la dharura na kipaumbele kisichoepukika
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i85768-raisi_kulinda_mazingira_ni_jambo_la_dharura_na_kipaumbele_kisichoepukika
Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika Mkutano wa Mawaziri wa eneo hili kuhusu ushirikiano wa mazingira kwa mustakabali bora kwamba; umuhimu wa mazingira unapasa kuzingatiwa na kwamba kila mmoja anapasa kulinda mazingira mbali na mitazamo ya kawaida, kidiplomasia na kisiasa.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 12, 2022 11:19 UTC
  • Raisi: Kulinda mazingira ni  jambo la dharura na kipaumbele kisichoepukika

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza katika Mkutano wa Mawaziri wa eneo hili kuhusu ushirikiano wa mazingira kwa mustakabali bora kwamba; umuhimu wa mazingira unapasa kuzingatiwa na kwamba kila mmoja anapasa kulinda mazingira mbali na mitazamo ya kawaida, kidiplomasia na kisiasa.

Mkutano wa Kikanda wa Mawaziri wa Maizngira wa Nchi za Magharibi mwa Asia umefanyika leo hapa Tehran kwa ubinifu wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ukihudhuriwa na Mawaziri na maafisa wa ngazi za juu wa nchi 11 za magharibi mwa Asia. Mkutano huo umefanyika lengo likiwa ni kuchunguza njia mbalimbali za kutatua matatizo ya mazingira katika eneo hili hasa tatizo la vumbi angani. 

Akihutubia leo mkutano huo hapa Tehran, Rais Sayyid Ebrahim Raisi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameeleza kuwa hii leo ni jambo lisiloepukika kulinda ekolojia na mazingira na ni daghadagha ya watu wote na nchi zote khususan nchi za kanda hii. 

Rais Raisi ameongeza kuwa kupenda makuu kwa mifumo ya uistikbari duniani, ugaidi na kuzizuia serikali na mataifa ya eneo kunufaika na elimu na teknolojia katika kuchukua maamuzi ndiyo sababu ya kushuhudiwa changamoto mbalimbali za mazingira hii leo.  

Rais wa Iran amesema, jambo lenye umuhimi miongoni mwa vizazi ni mazingira; na kulindwa kwake kunaweza kuandaa uwanja wa ushirikiano kati ya nchi rafiki na jirani. "Dunia hivi sasa inakabiliwa na matatizo mengi ya kimazingira nje ya mipaka ya kijiografia na kisiasa, na katika eneo la magharibi mwa Asia tunashudia athari za kimazingira ikiwa ni pamoja na vimbunga vya mchanga", amesema Rais wa Iran.

Kimbunga cha vumbi