Aug 05, 2022 01:15 UTC
  • Iran yawatia mbaroni wanachama wa ISIS waliotaka kushambulia maombolezo ya Muharram

Wizara ya Intelijensia ya Iran imetangaza habari ya kutiwa mbaroni wanachama kumi wenye mfungamano na Wazayuni wa kundi la kigaidi na kitakfiri la ISIS (Daesh).

Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa, vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu vimewatia nguvuni magaidi hao wa ISIS waliokuwa wanapanga njama ya kushambulia marasimu, mikusanyiko na vikao vya kumuomboleza Imam Hussein AS.

Wizara hiyo imesema magaidi hao wamekamatwa na vyombo vya usalama vya Iran katika maeneo mawili ya kusini na magharibi ya nchi wakila njama za kuvuruga maombolezo hayo ya mjukuu huyo wa Mtume Muhammad SAW katika mwezi huu mtukufu wa Muharram. 

Taarifa hiyo imebainisha kuwa, baada ya utawala wa Kizayuni kupata pigo kubwa wiki iliyopita kwa kutibuliwa njama zao batili, mara hii wamepata pigo jingine baada ya kukamatwa magaidi uliowatuma hapa nchini kuvuruga vikao vya kukumbuka mauaji ya Imam Hussein AS katika ardhi ya Karbala mwaka 61 Hijria.

Wizara ya Intelijensia ya Iran imeleeza kuwa, magaidi hao wenye mfungamano na utawala haramu wa Israel walikuwa na silaha, vyombo vya kisasa vya mawasiliano na mada za miripuko. Iran imefanikiwa kutwaa silaha hizo za maadui.

Makomandoo wa Iran

Wiki iliyopita, maafisa usalama wa Iran walifanikiwa kuvunja mtandao wa kundi la magaidi wanaotaka kujitenga wa Komoleh, ambao wanafadhiliwa na kuungwa mkono na Wazayuni.

Katika operesheni hiyo, vyombo vya usalama vya Jamhuri ya Kiislamu viliwatia nguvuni majasusi kadhaa waliokuwa wakitumikia shirika la ujasusi la Israel (Mossad), ambao walijipenyeza nchini kupitia eneo la Kurdistan, magharibi mwa Iran.  

Tags