Marandi: Iran haitakubali mianya na utata kuhusiana na mazungumzo ya Vienna
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i87856-marandi_iran_haitakubali_mianya_na_utata_kuhusiana_na_mazungumzo_ya_vienna
Mshauri wa timu ya Iran katika mazungumzo ya Vienna amesisitiza kuwa Iran haitakubali mianya na utata kuhusiana na mazungumzo hayo.
(last modified 2025-10-19T03:07:26+00:00 )
Sep 06, 2022 07:57 UTC
  • Marandi: Iran haitakubali mianya na utata kuhusiana na mazungumzo ya Vienna

Mshauri wa timu ya Iran katika mazungumzo ya Vienna amesisitiza kuwa Iran haitakubali mianya na utata kuhusiana na mazungumzo hayo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ISNA Mohammad Marandi, ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter: "Borrell ni mshirika wa Marekani na anasahau kuwa sababu ya mazungumzo haya ni ukiukaji wa JCPOA uliofanywa na nchi za Magharibi na mashinikizo ya vikwazo vya kiwango cha juu kabisa ambavyo vinawalenga raia wa Iran, hata pale Iran ilipotekeleza kikamilifu JCPOA."
Marandi ameongezea kwa kusema: "Iran haitakubali mianya na utata; Marekani inaubebesha gharama Umoja wa Ulaya."
Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema katika mkutano na waandishi wa habari kwamba, ana matumaini madogo hivi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma juu ya kufikiwa mwafaka huko Vienna wa kufufua makubaliano ya nyuklia ya JCPOA.
Josep Borrell

Borrell amedai kwamba, badala ya kukaribiana, maoni juu ya makubaliano ya nyuklia ya Iran yanazidi kuachana na kuwa mbali.

Hivi karibuni Marekani na Iran zimekuwa zikihakiki majibu ya kila mmoja wao kuhusu hati ya mapendekezo ya Umoja wa Ulaya ya kufufua mapatano ya nyuklia, ambayo kwa mujibu wa Josep Borrell, ambaye ndiye mratibu wa mazungumzo, hiyo ndiyo hati rasmi na pendekezo la mwisho la kufufua makubaliano hayo ya JCPOA.
Tarehe 8 Mei 2018, Marekani ilijiondoa rasmi katika mapatano ya JCPOA ambapo mbali na kurejesha vikwazo vya zamani, iliiwekea Iran vikwazo vingine vipya.
Baada ya Marekani kujitoa katika JCPOA na kuiwekea vikwazo Tehran, nchi za Ulaya ziliahidi kubaki na kuyaendeleza kikamilifu mapatano hayo ya pande kadhaa, lakini hazikutekeleza hata moja kati ya ziliyoyaahidi.../