Mwandishi wa habari wa Marekani amuenzi Shahidi Kamanda Qassem Soleimani
https://parstoday.ir/sw/news/iran-i92542-mwandishi_wa_habari_wa_marekani_amuenzi_shahidi_kamanda_qassem_soleimani
Mwandishi wa habari Mmarekani Gilda Morkert, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa tatu tangu alipouawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, akizienzi juhudi za shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ugaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 05, 2023 22:51 UTC
  • Mwandishi wa habari wa Marekani amuenzi Shahidi Kamanda Qassem Soleimani

Mwandishi wa habari Mmarekani Gilda Morkert, ameandika ujumbe kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa tatu tangu alipouawa shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, akizienzi juhudi za shujaa huyo wa mapambano dhidi ya ugaidi.

Katika maadhimisho ya mwaka wa tatu wa kukumbuka siku aliyouawa Shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, shakhsia wengi wa kisiasa na wa vyombo vya habari duniani wamemuezi kamanda huyo na nafasi na mchango mkubwa aliotoa hususan katika mapambano dhidi ya makundi ya kigaidi na hasa dhidi ya kundi la kigaidi la DAESH (ISIS).
Gilda Morkert, mwandishi wa habari wa Marekani, ameweka picha ya Haj Qassem Soleimani kwenye mtandao wa Twitter na kuandika: "ninaienzi kumbukumbu ya shujaa azizi Soleimani, na ningependa kuiadhimisha adhama yake kwa muda wa wiki yote hii".
Hivi karibuni, Sara Flounders, mkuu wa kundi linalopinga vita la Marekani na mjumbe wa bodi ya wakurugenzi ya Kamati ya Uratibu wa Kimataifa ya Kupinga Ubeberu, aliisifu shakhsia ya Jenerali Soleimani na kusema: "japokuwa sijawahi kukutana na Qassem Soleimani, ninachojua ni kwamba akiwa kiongozi wa kisiasa na kijeshi wa Iran, aliitetea Palestina na muqawama wote katika eneo na hata nchi zingine kama Venezuela".

Shahidi Kamanda Luteni Jenerali Qassem Soleimani

Gazeti la Uingereza la Sun, katika makala yake iliyobainisha kuwa serikali ya Marekani daima imekuwa ikiunga mkono ugaidi, limesisitiza kwamba lengo la kumuua Shahidi Luteni Jenerali Hajj Qassem Soleimani na Abu Mahdi Al-Muhandis ni kuchelewesha mwisho wa ubeberu wa Marekani duniani.
Gazeti hilo la Uingereza limeongeza kuwa: "jinai iliyofanywa uwanja wa ndege wa Baghdad ilikuwa sawa na kuiondoa amani na kuimarisha ugaidi kwa lengo la kurejesha maslahi ya Marekani."

Luteni Jenerali Qassem Soleimani, aliyekuwa kamanda wa Kikosi cha Quds cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu, aliuawa shahidi Januari 3, 2020 katika shambulio la anga lililofanywa na jeshi vamizi na la kigaidi la Marekani karibu na uwanja wa ndege wa Baghdad, akiwa pamoja na Abu Mahdi Al-Muhandis, Naibu Mkuu wa harakati ya kujitolea ya wananchi wa Iraq ya Al-Hashd al-Shaabi na wanamapambano wengine wanane, wakati alipoelekea Iraq kwa mwaliko rasmi wa viongozi wa nchi hiyo.../