Meja Jenerali Mousavi: Uwezo wa droni za jeshi la Iran unaongezeka
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesisitiza kuwa ndege zisizo na rubani zina nafasi kubwa katika vita na kwamba kuwepo aina tofauti za ndege hizo hapa nchini kunaongeza uwezo wa kufanya maamuzi wa kamanda katika medani ya vita.
Ameongea kuwa: Nguvu ya ndege zisizo na rubani za jeshi la Iran. zinaongezeka kwa idadi na ubora.
Meja Jenerali Sayyid Abdulrahim Mousavi Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria maendeleo ya Jeshi la Ulinzi wa Anga na kusema kuwa: Wakati fulani kulikuwa na wasiwasi juu ya upungufu wa rada kwenye mipaka ya nchi lakini leo hii hakuna tena wasiwasi kuhusu suala hilo.
Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amekumbusha kuhusu uwezo wa ndege zisizo na rubani za jeshi na kuongeza kuwa: Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran huko nyuma pia lilikuwa na droni lakini kuanzia mwaka mmoja hadi miwili iliyopita nguvu hii imejulikana kwenye vyombo vya habari kupitia maneva ya kijeshi ya ndege zisizo na rubani yanayofanyika hapa nchini.
Meja Jenerali Mousavi ameeleza kuwa, kuna wakati vijana wa Kiirani hawakuruhusiwa kujifunza masuala ya kiufundi ya kijeshi lakini hivi sasa vijana hao wanaunda ndege wao wenyewe. Amesema, kwa mujibu wa nyaraka zote zilizopo, tangu siku ya kwanza ya Mapinduzi ya Kiislamu hapa nchini hadi sasa, kila kazi liliyopewa Jeshi la Anga imefanywa kwa njia bora zaidi.
Hafla ya makabidhiano ya zaidi ya ndege zisizo na rubani 200 za aina ya Karar, Ababil 4 na 5, Arash na nyinginezo imefanyika hapa Tehran na katika baadhi ya mikoa ya Iran mbele ya Kamanda Mkuu wa Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na Waziri wa Ulinzi.