Iran: Mitazamo ya umma ya Wamarekani inabadilika kuhusu ubaguzi wa rangi Israel
Iran imeangazia "mabadiliko yanayoonekana" katika maoni ya umma wa Marekani kuhusu hali ya ubaguzi wa rangi au mfumo wa apathaidi katika utawala haram Israel, ikitoa mfano wa uchunguzi wa maoni uliofanyika hivi karibuni Marekani amba unaonyesha namna utawala huo ghasibu uliovypoteza uungaji mkono Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Nasser Kan'ani, alisema hayo katika ujumbe wa Twitter siku ya Jumapili kwamba : "Uchunguzi wa karibuni wa Chuo Kikuu cha Maryland umebaini kuwa asilimia 44 ya Wademokrat na asilimia 20 ya Warepublican wanaamini kuwa Israel ni "utawale wenye ubaguzi ubaguzi sawa na mfumo wa apathaidi .”
Kanani amesema ni wazi kuwa pamoja na kuwa Marekani ni muungaji mkono mkuu wa utawala bandia wa Israel, Wamarekani wengi wanautazama utawala huo kuwa ni wa ubaguzi wa rangi.
Katika uchunguzi huo, uliofanywa kuanzia tarehe 27 Machi hadi 5 Aprili 2023 kati ya waliohojiwa 1,203, asilimia 41 ya Wanademokrasia walisema wanaunga mkono vuguvugu la Kuisusia, Kuitenga na Kuiwekaa Vikwazo Israel (BDS).
Vuguvugu la BDS linalenga kukabiliana na ukatili na ukandamizaji wa miongo kadhaa wa Israel dhidi ya Palestina kupitia kuususia utawala huo sawa na kampeni zilizofanikiwa za kususia utawala wa apathaidi au ubaguzi wa rangi Afrika Kusini.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: "Hakika kutakuwa na matokeo ya kushangaza zaidi kuhusu uwepo wa utawala bandia wa Israel iwapo watu wataruhusiwa kuwa na uhuru u wa kujieleza dhidi ya Wazayuni." Amesema kwa sasa uhuru wa kujielza Marekani kuhusu Wazayuni umebanwa kutokana na ushawishi wa makundi ya Kizayuni.
Utafiti huo unakuja huku kukiwa na mvutano mkali kati ya baraza la mawaziri la mrengo wa kulia la Israel linaloongozwa na waziri mkuu Benjamin Netanyahu na serikali ya rais wa Marekani Joe Biden.
Shibley Telhami, mkurugenzi wa Kura ya Masuala Muhimu katika Chuo Kikuu cha Maryland amesema ni wazi kwamba mitazamo ya umma kuhusu Israeli inabadilika. Neno ‘ubaguzi wa rangi’ linaonekana kuwa neno la kawaida miongoni mwa Wamarekani wengi, hasa Wademokrat.
"Na hata vuguvugu la BDS, ambalo limekabiliwa na vizuizi vingi katika jamii kuu ya Marekani, linaonekana kuwa na uungwaji mkono mkubwa kati ya Wanademokrasia ambao walitoa maoni yao."