Wairani wanaadhimisha Siku ya Ghuba ya Uajemi, wasisitiza majina bandia hayatabadilisha ukweli
Wananchi wa Iran leo wameadhimisha Siku ya Kitaifa ya Ghuba ya Uajemi, ambayo ni nembo ya misimamo isiyoyumba ya kukabiliana na njama za baadhi ya nchi za kikanda za kutaka kubadilisha jina la eneo hilo la kistratijia la maji.
Ikiashiria siku hii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran iliandika katika chapisho kwenye ukurasa wake rasmi wa Twitter kwamba "Wairani wanaadhimisha Aprili 30 kama "SikuYaGulfYaUajemi. (#PersianGulfDay) "
Taarifa hiyo kupitia ujumeb wa Twitter imeendelea kusema: "Jina la 'Ghuba ya Uajemi' limezaliwa na historia. Vyanzo vyote vya kihistoria na kimataifa, ramani za kale, nyaraka, vitabu pamoja na maagizo ya Umoja wa Mataifa vinathibitisha kwamba maji yaliyoko kusini mwa Iran yamekuwa yakiitwa Ghuba ya Uajemi (#PersianGulf),” ilisoma tweet hiyo.
Wakati huo huo, Wairani wamenyanyua mabango na mabango mbele ya balozi za Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na Uingereza katika mji mkuu wa Tehran, kupinga hatua ya maafisa wa nchi hizo mbili kutumia jina bandia badala ya Ghuba ya Uajemi.
Ghuba ya Uajemi - ambayo ina urefu wa kilomita za mraba 251,000 - inapakana na Mto Arvand upande wa kaskazini, ambao ni mpaka kati ya Iran na Iraqi, na Mlango Bahari wa Hormuz kusini, unaounganisha Ghuba ya Uajemi na Bahari ya Oman na Bahari ya Hindi.
Bahari ya kimkakati Ghuba ya Uajimi ni njia ya biashara ya kimataifa inayounganisha Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) na Afrika, India, na China
Imetajwa na wanahistoria na maandishi ya kale kama bahari ya "Kiajemi" tangu Milki ya Achaemenid ilipoanzishwa katika eneo ambalo sasa ni Iran ya kisasa.
Kila mwaka, Wairani huadhimisha Siku ya Ghuba ya Uajemi tarehe 10 Ordibehesht, mwezi wa pili kwenye kalenda ya Kiirani ya Hijria Shamshia, ambayo kwa kawaida huwa Aprili 30.
Tarehe hiyo inasdifiana na siku ya kampeni ya kijeshi yenye mafanikio ya Shah Abbas wa Kwanza mwaka wa 1622, ambayo ilipekea kutimuliwa jeshi la wanamaji la Ureno katika eneo la Mlango Bahari wa Hormuz.
Ingawa nyaraka za kihistoria zinaonyesha kwamba eneo hilo la bahari daima imekuwa ikijulikana kama "Ghuba ya Uajemi," baadhi ya mataifa ya Kiarabu na washirika wao mara kwa mara hutumia jina bandia la "Ghuba ya Arabia" kuashiria bahari hiyo.