Balozi wa Kenya Iran atembelea "Bustani ya Makumbusho ya Naderi" mjini Mashhad
Balozi wa Kenya nchini Iran ametembelea Jumba la Bustani ya Makumbusho ya Naderi lililoko mjini Mashhad, Mkoa wa Khorasan Razavi.
Jumba la kumbukumbu la kiutamaduni na kihistoria la Bagh-Naderi Museum liko kwenye makutano ya barabara ya Mashahidi wa Mashhad umbali wa mita 500 kutoka mahali ilipo haram tukufu ya Imam Reza AS.
Kaburi la Nader liko katika sehemu kuu ya Ibn Bagh ya makumbusho hiyo na kando ya kaburi hilo, kuna kumbi kuu mbili.
Moja ya kumbi hizo ni Jumba la Makumbusho la Silaha za Kale, ambapo silaha za zama tofauti za historia ya Iran zinaonekana katika jumba hilo la makumbusho.
Halikadhalika, picha za uchoraji zilizopambwa kwa taswira za Nader Shah akiwa vitani na nyaraka za hati maridadi zilizoandikwa kwa mkono ikiwemo historia ya safari za dunia za Naderi ni turathi zingine adhimu za kihistoria zilizoko katika makumbusho hayo.
Ukumbi mwingine ni wa makumbusho ya athari, nyaraka na vifaa vya utawala wa Nader Shah.
Katika makumbusho hiyo kuna kaburi pia la Kanali Mohammad Taqi Khan Pesian, jemadari mzalendo wa Iran.../