-
Iran yatoa pigo kubwa la kihistoria kwa Israel
Jun 07, 2025 14:08Shirika la habari la IRIB limenukuu duru za kuaminikia katika eneo hili la Asia Magharibi zikisema kuwa, taasisi ya kiintelijensia ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa pigo kubwa kwa Israel. Imefanikiwa kuhamisha kutoka kwa utawala wa Kizayuni taarifa za siri za kijasusi, nyeti na za kiistratijia ikiwemo miradi na taasisi za atomiki za Israel.
-
Aragchi: Iran haitaki kumiliki silaha za nyuklia
Jun 07, 2025 09:35Seyed Abbas Araghchi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, amesisitiza kwa mara nyingine kuwa Iran haina nia yoyote ya kumiliki silaha za nyuklia, akieleza kwamba msimamo wa Iran umejengwa juu ya misingi ya kidini pamoja na fatwa ya wazi iliyotolewa na Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Seyyed Ali Khamenei.
-
Iran yalaani hatua ya kibaguzi ya Marekani ya kuwapiga marufuku Waislamu kuingia nchini humo
Jun 07, 2025 09:23Tehran imelaani vikali amri ya Rais wa Marekani, Donald Trump, ya kuwapiga marufuku wananchi wa Iran na raia kutoka mataifa mengine yenye Waislamu wengi kuingia Marekani, ikisema hatua hiyo inaonesha uadui wa kina wa Washington dhidi ya Wairani.
-
Iran, Imarati zasisitiza haja ya Waislamu kote duniani kuwa na umoja
Jun 07, 2025 03:30Rais Masoud Pezeshkian wa Iran na Kiongozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan wametoa wito wa umoja wa Waislamu.
-
Araqchi ayaonya madola ya Ulaya: Iran itajibu kwa nguvu ukiukaji wowote wa haki zake
Jun 06, 2025 23:02Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araqchi amezionya nchi za Ulaya dhidi ya kuchukua hatua zozote ovu dhidi ya Iran kwenye Bodi ya Magavana ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) na kusisitiza kwamba, Tehran itajibu kwa nguvu ukiukaji wowote wa haki zake.
-
Abu Torabi Fard: Imam Khomeini ameugeuza Umma wa Kiislamu kuwa nguvu mpya duniani
Jun 06, 2025 03:19Khatibu wa Sala ya Idul Adh'ha iliyosaliwa leo hapa mjini Tehran amesema: Imam Khomeini (MA) alifanikiwa kuleta mageuzi makubwa nchini Iran na pia kuugeuza Umma wa Kiislamu kuwa nguvu mpya inayozidi kunawiri kwenye ulimwengu wa leo.
-
Baqaei: Kujaribu kuhalalisha jinai za kutisha za Israel ni janga kubwa zaidi duniani leo
Jun 06, 2025 03:18Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema: Kujaribu kuhalalisha jinai za kutisha na mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wananchi wasio na ulinzi wa Palestina, ni janga kubwa zaidi duniani leo, na kwamba waungaji mkono wa jinai hizo na wahalalishaji wa uhalifu wa kuchupa mipaka wa utawala wa Kizayuni ni washirika wa moja kwa moja wa jinai za Israel.
-
Iran yaishtaki IAEA kwa madai yake yasiyo na msingi
Jun 06, 2025 03:17Iran imetoa hati ya kisheria kupinga madai ya “ujasusi” ya Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA na kuyataja kuwa ni ya kichochezi na yasiyo na msingi. Tehran inaamini kuwa shirika hilo limevuka mipaka yake na linatoa matamshi dhidi ya Iran kwa kutegemea ushahidi bandia.
-
Pezeshkian: Iran ina nia ya kweli ya kuimarisha ushirikiano na nchi zote za Kiislamu
Jun 05, 2025 23:00Rais Masoud Pezeshkian amefanya mazungumzo ya simu na Mrithi wa Kiti cha Ufalme wa Saudi Arabia, na sambamba na kumpa mkono wa Idi kwa mnasaba wa sikukuu ya Idul Adh’ha amesisitizia udharura wa kuendelezwa uhusiano wa kidugu kati ya nchi hizi mbili za Kiislamu, kuzidisha ushirikiano wa kieneo na kuimarisha umoja na mshikamano wa mataifa yote ya Waislamu.
-
Imam Khomeini: Urithi wa uongozi wa kidini na kimapinduzi
Jun 05, 2025 06:55Katika mwaka wa 36 wa maadhimisho ya kuaga dunia Imam Ruhollah Khomeini (MA), mwanzilishi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini Iran, fikra zake zingali zinaendelea kuathiri sio tu mwelekeo wa kisiasa wa Jamhuri ya Kiislamu bali pia mijadala mipana zaidi kuhusu mahusiano kati ya Uislamu na siasa katika ulimwengu wa Kiislamu.