-
Rais wa Iran: Undumakuwili wa Marekani umeipa Israel kiburi cha kutenda jinai za kutisha na kuhatarisha amani
Aug 12, 2024 04:36Rais wa Iran Masoud Pezeshkian amesema sera za undumakuwili za Marekani na baadhi ya nchi za Ulaya zimeupa moyo zaidi utawala wa Kizayuni wa Israel wa kutekeleza jinai mbaya zaidi huko Gaza na katika eneo zima.
-
China yatangaza kuunga mkono Iran katika kulinda usalama wake
Aug 12, 2024 04:35Waziri wa Mambo ya Nje wa China Wang Yi anasema Beijing inaiunga mkono Iran katika kutetea "mamlaka yake, usalama na heshima ya taifa" huku Tehran ikiahidi kuiadhibu vikali Israel kutokana na mauaji ya Ismail Haniyeh, mkuu wa ofisi ya kisiasa ya harakati ya Hamas.
-
Iran: Israel haitaweza katu kufidia vipigo vya kushindwa ilivyopata tangu Kimbunga cha Al-Aqsa hadi sasa
Aug 11, 2024 23:39Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, licha ya jinai na mauaji ya kutisha uliyofanya dhidi ya Wapalestina, Utawala wa Kizayuni wa Israel hautaweza katu kufidia vipigo vya kushindwa kistratejia ulivyopata tangu ilipotekelezwa Operesheni ya Kimbunga cha Al-Aqsa hadi sasa.
-
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Iran: Taasisi za kimataifa ni washirika katika jinai za utawala wa Kizayuni
Aug 11, 2024 07:57Makamu wa Kwanza wa Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kuwa taasisi za kimataifa zinashiriki katika jinai za utawala wa Kizayuni.
-
Iran: Hatutaruhusu Israel ichochee moto wa vita Asia Magharibi
Aug 11, 2024 04:05Kaimu Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesema Jamhuri ya Kiislamu inafanya hima kuzuia utawala wa Kizayuni wa Israel utimize ndoto yake ya kuwasha na kuchochea moto wa vita vya pande zote katika eneo la Asia Magharibi.
-
Qalibaf: Israel haielewi lugha nyingine isipokuwa ya mabavu
Aug 11, 2024 04:03Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge) amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu imedhamiria kujibu mapigo kwa Israel kufuatia mauaji ya kigaidi ya Ismail Haniyah, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS hapa Tehran akisisitiza kuwa, utumiaji wa nguvu na mabavu ndiyo njia pekee ya kukabiliana na Uzayuni.
-
Rais wa Iran ataka dunia kulinda amani, kuzuia jinai za Israel dhidi ya ubinadamu
Aug 11, 2024 02:16Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Masoud Pezeshkian amesema mashirika ya kimataifa hususan Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lazima yatimize wajibu wao wa kulinda amani na usalama wa kieneo na dunia na kuzuia jinai dhidi ya binadamu zinazotekelezwa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Iran yalaanii vikali jinai mpya za utawala wa Kizayuni kwenye Ukanda wa Ghaza
Aug 11, 2024 02:14Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani vikali jinai nyingine ya kutisha iliyofanywa na Israel katika shule moja kwenye kambi ya wakimbizi wa Palestina na amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua za haraka za kuudhibiti utawala katili wa Kizayuni.
-
Iran: Tumeshaandaa mazingira ya kutoa jibu kali dhidi ya Israel
Aug 10, 2024 10:13Mshauri wa masuala ya kisiasa wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Ali Khamenei amesema mazingira yameshaandaliwa kwa ajili ya Iran kutoa jibu kali na la kuumiza dhidi ya Israel, kutokana na hatua ya utawala huo wa Kizayuni kumuua shahidi Ismail Haniyah, Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina HAMAS.
-
Iran yakadhibisha madai ya kutaka kuingilia uchaguzi wa Marekani
Aug 10, 2024 07:42Ofisi ya uwakilishi wa kudumu ya Iran katika Umoja wa Mataifa imepuuzilia mbali madai kuwa Jamhuri ya Kiislamu inakula njama ya kuathiri matokeo ya uchaguzi wa rais wa Marekani utakaofanyika baadaye mwaka huu.