-
Mkuu wa Majeshi ya Iran: Marekani, Israel zilishindwa kudhoofisha uwezo wa Iran wa nyuklia, makombora na ulinzi wa anga
Sep 07, 2025 03:07Mkuu wa Majeshi ya Iran, Meja Jenerali Amir Hatami, amesema Marekani na utawala wa Israel zililenga kudhoofisha uwezo wa nyuklia, makombora na ulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu wakati wa vita vya siku 12 mwezi Juni mwaka huu, lakini walishindwa kufikia malengo yao makuu.
-
Araghchi: Iran na IAEA zinakaribia kuunda fremu mpya ya ushirikiano
Sep 06, 2025 23:20Iran imesema imekaribia sana kubuni mfumo mpya wa ushirikiano baina yake na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA), miezi kadhaa baada ya mashambulizi ya anga ya Israel na Marekani dhidi ya vituo vya nyuklia vya nchi hii kuipelekea Tehran kusimamisha ushirikiano wake na taasisi hiyo ya Umoja wa Mataifa.
-
Sambamba na kuanza duru mpya ya mazungumzo, Iran yatilia mkazo diplomasia katika kadhia ya nyuklia
Sep 06, 2025 03:31Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araghchi amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa liidhinishe juhudi za kidiplomasia katika kushughulikia mpango wa nyuklia wa Tehran na kukomesha vitendo vya "kinyume na sheria" vya Ulaya.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran: Sutafahamu zilizotokea baina yetu na Qatar zimeondolewa
Sep 05, 2025 23:36Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Abbas Araghchi amesema, mazungumzo yake na viongozi wa Qatar yalikuwa yenye faida na mafanikio makubwa na yalifanyika kwa uzito maalumu na akaongezea kwa kusema: "kwa bahati nzuri, hakuna tofauti zozote kati ya nchi hizi mbili, na sutafahamu iliyojitokeza imetatuliwa kikamilifu na ziara hii".
-
"Hatua ya nchi za Ulaya kuamilisha utaratibu wa snapback ni ya kiholela"
Sep 05, 2025 08:38Khatibu wa Muda wa Swala ya Ijumaa iliyoswalia leo hapa Tehran amesema: Kwa mujibu wa taarifa ya mwisho ya Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai, jaribio lolote la kubadilisha Azimio Nambari 2231 linadhoofisha itibari ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kwamba hatua ya nchi tatu za Ulaya ya kuamilisha utaratibu wa "snapback" wa kurejesha vikwazo vya baraza hilo dhidi ya Iran ni ya kiholela.
-
IRGC: Adui hana ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran
Sep 05, 2025 07:33Msemaji wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran (IRGC) amesema Israel na washirika wake hawana uwezo wala ubavu wa kuanzisha vita vipya dhidi ya Iran, hivyo basi, wamekimbilia operesheni za vita vya kisaikolojia.
-
Iran yaitaka dunia ilaani mashambulizi dhidi ya vituo vyake vya nyuklia
Sep 05, 2025 07:32Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Iran amesema Marekani na utawala wa Israel zilifanya mashambulizi ya kimakusudi dhidi ya vituo vya nyuklia ya Iran, licha ya vituo hivyo kuwa chini ya usimamizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kudhibiti Nyuklia.
-
Araqchi: 'Iran itaendelea kuunga mkono Muqawama wa Palestina dhidi ya Israel'
Sep 05, 2025 03:37Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Iran amesisitiza dhamira ya nchi hiyo ya kuunga mkono Muqawama halali na mapambano ya watu wa Palestina dhidi ya utawala vamizi wa Israel hadi pale haki zao zitakaporejeshwa kikamilifu.
-
Ripoti: Takriban Wairani 100 walikuwa wahanga wa ugaidi katika mwaka uliopita wa Kiajemi
Sep 04, 2025 22:52Mashambulizi ya kigaidi yaligharimu maisha ya takriban Wairani mia moja katika mwaka uliopita wa kalenda ya Kiirani, uliomalizika Machi 20. Hii ni kwa mujibu wa ripoti mpya ya shirika lisilo la kiserikali linalowakilisha familia za wahanga Wairani wa mashambulizi ya kigaidi.
-
Araqchi: IAEA imeafiki haja ya mfumo mpya wa ushirikiano na Iran
Sep 04, 2025 22:49Sayyid Abbas Araqchi Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amesisitiza kuwa hakutakuwa na ushirikiano mpya baina ya Iran na Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) hadi hapo mazungumzo yatakapokamilika.