-
Iran yalipiza kisasi: Balozi wa Australia aondoka Tehran
Sep 04, 2025 11:12Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran ametangaza kwamba balozi wa Australia mjini Tehran ameondoka nchini na kuongeza kuwa: "Kwa mujibu wa kaida na sheria za kidiplomasia, katika kukabiliana na hatua ya Australia ya kumfukuza balozi wa Iran mjini Canbera, Jamhuri ya Kiislamu imejibu mapigo kwa kupunguza kiwango cha uhusiano wa kidiplomasia wa Australia nchini Iran."
-
Waziri wa Ulinzi wa Iran: Jumuiya ya Shanghai inaweza kuasisi miungano ya usalama yenye ufanisi
Sep 04, 2025 10:33Waziri wa Ulinzi wa Iran, Brigedia Jenerali Aziz Nasirzadeh amesema kuwa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai (SCO) ina uwezo wa kupanua wigo wa shughuli zake na kuanzisha miungano ya usalama yenye ufanisi katika siku zijazo.
-
Araghchi: Iran haiogopi mazungumzo, wala vita
Sep 04, 2025 04:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi amesema Jamhuri ya Kiislamu haiogopi kuingia katika mazungumzo mapya kuhusu utatuzi wa masuala yoyote yaliyopo, kama ambavyo haina hofu ya kuingia katika vita vyovyote vipya ambavyo vinaweza kutwishwa nchi hii na maadui zake.
-
Ghana kufungua tena Ubalozi wake Tehran mwezi huu wa Septemba
Sep 04, 2025 04:10Wizara ya Mambo ya Nje ya Ghana imesema kuwa Ubalozi wake hapa mjini Tehran, Iran, utaanza tena kazi zake Jumanne ya Septemba 16, baada ya kufungwa kwa muda.
-
Marekani inafutilia nini katika kuweka vikwazo vipya dhidi ya Iran?
Sep 04, 2025 03:51Marekani imeweka vikwazo vipya ili kuzuia uuzaji nje wa mafuta ya Iran.
-
Tehran yampongeza mbunge wa Ireland kwa kuangazia mauaji ya kimbari ya Israel huko Gaza, shambulio dhidi ya Iran
Sep 03, 2025 23:44Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baqaei, amempongeza mbunge wa kujitegemea wa Ireland katika Bunge la Ulaya (MEP) kwa kuangazia jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza na kulaani mashambulizi ya utawala huo dhidi ya Iran mwezi Juni. Baqaei ameutaka Umoja wa Ulaya kuiga mfano huo.
-
Pezeshkian ataka Iran na China zishirikiane katika kupinga ubabe wa kimataifa
Sep 03, 2025 09:55Rais Masoud Pezeshkian wa Iran, amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na China katika kupinga vitisho na ushawishi wa upande mmoja kutoka kwa mataifa yanayojaribu kuvuruga uhusiano wa kirafiki kati ya nchi hizi mbili.
-
Larijani: Marekani inazuia njia ya mazungumzo na Iran kwa kuibua madai yasiyotekelezeka
Sep 03, 2025 09:45Afisa mkuu wa usalama wa Iran amesema kuwa Marekani inazuia mazungumzo yanayoweza kufanyika kwa kuibua “madai yasiyotekelezeka,” ikiwa ni pamoja na kuweka vizuizi dhidi ya mpango wa makombora wa Iran.
-
Makubaliano ya Iran na China; njia ya kuondokana na uchukuaji maamuzi ya upande mmoja
Sep 03, 2025 05:17Katika kikao chao, Marais wa Iran na China, Masoud Pezeskian na Xi Jinping wameashiria uwezo, misingi na matakwa ya viongozi wa nchi hizo mbili ya kupanua ushirikiano, na kusisitiza maslahi na utayari wao wa kuboresha uhusiano kwa kuangalia mustakabali, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa kiwango cha juu zaidi wa makubaliano ya kimkakati ya miaka 25 kati yao.
-
Spika wa Iran: Waislamu wana wajibu wa kukomesha mauaji ya Israel Gaza
Sep 03, 2025 03:43Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran) ameyataka mataifa ya Kiislamu kuungana katika vita dhidi ya utawala wa Kizayuni, ambao ameutaja kuwa shetani mkubwa zaidi duniani.