-
Jibu la Caracas kwa Trump katika Umoja wa Mataifa
Dec 21, 2025 06:08Mwakilishi wa kudumu wa Venezuela katika Umoja wa Mataifa amelaani madai ya Rais Donald Trump kwamba Marekani inamiliki eneo la nchi hiyo na rasilimali za mafuta, akionya kwamba enzi ya ukoloni wa kale imekwisha.
-
Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa: Misri inaunga mkono mauaji ya halaiki ya Wapalestina
Dec 21, 2025 06:04Ripota Maalum wa Umoja wa Mataifa ameitaja hatua ya Misri ya kuidhinisha makubaliano ya ununuzi wa gesi kutoka kwa utawala wa Israel kuwa ni uungaji mkono wa nchi hiyo kwa mauaji ya halaiki ya Wazayuni huko Gaza.
-
Bunge la Algeria laanza kujadili muswada wa kujinaisha ukoloni wa Ufaransa
Dec 21, 2025 05:42Bunge la Algeria jana lilifungua mjadala kuhusu rasimu ya sheria inayotaka kujinaisha utawala wa kikoloni wa Ufaransa nchini humo kati ya mwaka 1830 na 1962.
-
Kwa nini mpango wa Al‑Ahram kuhusu usalama wa Asia Magharibi ni wa kupotosha na ni hatari?
Dec 21, 2025 04:27Tovuti ya Ahram Online (sehemu ya Kiingereza ya gazeti la Al-Ahram la Misri) katika makala yake imependekeza kufanyika kwa mkutano wa usalama katika eneo la Asia ya Magharibi, kwa ushiriki wa madola yenye nguvu zaidi duniani, ili kuzuia kuanza tena kwa vita kati ya Iran na utawala wa Kizayuni wa Israel.
-
Picha za satelaiti zaonyesha Israel ikijimarisha kuwepo kijeshi katika Ukanda Gaza
Dec 21, 2025 04:26Utawala wa Israel unaonekana kuandaa mazingira ya kudumisha uwepo wake kijeshi katika maeneo makubwa ya Ukanda wa Gaza. Hii ni kwa mujibu wa uchambuzi mpya wa picha za satelaiti ulioweka wazi ujenzi mkubwa, upanuzi wa miundombinu na kuendelea kuharibiwa mali za Wapalestina tangu kutekelezwa mapatano ya usitishaji vita mwezi Oktoba.
-
Marekani yazuia meli nyingine ya mafuta kutoka Venezuela huku ikizidisha mashinikizo dhidi ya Caracas
Dec 21, 2025 04:22Wanajeshi wa Marekani wameisimamisha meli nyingine ya mafuta ya Venezuela katika pwani ya nchi hiyo ikiwa ni operesheni ya pili ya aina hiyo ndani ya wiki mbili, huku Rais Donald Trump wa Marekani akiendelea na kampeni kali inayolenga kuzidisha mashinikizo kwa serikali ya Rais Nicolas Maduro.
-
Lavrov: Kuimarishwa usalama ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya Afrika
Dec 21, 2025 04:16Sergei Lavrov Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema kuwa kuimarisha amani na usalama barani Afrika ni jambo muhimu ili kuhakikisha ustawi wa bara hilo na maendeleo endelevu, na ni kipengee muhimu katika kudumisha amani duniani.
-
Ufyatuaji risasi Afrika Kusini; watu wenye silaha waua 9 karibu na Johannesburg
Dec 21, 2025 04:13Watu waliokuwa na silaha, usiku wa kuamkia leo, wamefyatua risasi kiholela katika kitongoji kimoja karibu na Johannesburg nchini Afrika Kusini na kuua takriban watu 9 na kujeruhi wengine kadhaa.
-
Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi: Utawala wa Israel unaficha kushindwa kwa kutoa vitisho
Dec 20, 2025 23:38Brigedia Jenerali Ahmad Vahidi, Naibu Mkuu wa Majeshi ya Iran, amesema "Israel" inajaribu kuficha kushindwa vikali katika Vita vya Siku Kumi na Mbili kupitia njia ya kutoa vitisho, propaganda za vyombo vya habari na ujanja wa kisiasa.
-
Kikao cha Brussels na kurudi nyuma Ulaya inayosokotwa na tofauti za ndani, katika mpango wake wa unyang'anyi wa mali za Russia
Dec 20, 2025 23:09Licha ya viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuandamwa na mashinikizo ya kisiasa ya Marekani ya kuwataka watoe msukumo wa kuvipatia suluhisho la haraka vita vya Ukraine, viongozi hao waliokutana kwenye makao makuu ya umoja huo mjini Brussels, wameamua kurudi nyuma na kulegeza msimamo katika uchukuaji uamuzi wenye gharama kubwa na hasi wa kunyakua mali za Russia,