-
Benin yamtia mbaroni waziri wa zamani wa ulinzi kwa jaribio la mapinduzi lililoshindwa
Dec 20, 2025 23:08Benin, jana Jumamosi, ilimuweka kizuizini waziri wa zamani wa ulinzi na kiongozi wa upinzani, Candide Azannai, kama sehemu ya uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi lililoshindwa mapema mwezi huu.
-
Mahakama Kuu ya UN kusikiliza kesi ya mauaji ya kimbari dhidi ya Waislamu wa Myanmar, mwezi Januari
Dec 20, 2025 23:07Mahakama Kuu ya Umoja wa Mataifa mwezi Januari mwakani itafanya vikao vya hadhara kuhusu mauaji ya kimbari ya Waislamu nchini Myanmar ya mwaka 2017.
-
Mjumbe wa UN: Hali ya usalama bado ni tete katika mji mkuu wa Libya,Tripoli
Dec 20, 2025 23:06Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na masuala ya Libya amesema kuwa hali ya usalama huko Tripoli imeboreka kwa kiasi fulani kufuatia mipango mipya ya usalama, hata hivyo ametahadharisha kuwa ukosefu wa usalama unaendelea kushuhudiwa katika mji huo mkuu na katika mikoa ya magharibi mwa Libya.
-
Ripoti: Watoto wa Gaza wanateseka na baridi kali
Dec 20, 2025 23:05Dhoruba za majira ya baridi kali zimesababisha vifo vya Wapalestina wasiopungua 17 katika Ukanda wa Gaza mwezi huu wa Disemba pekee.
-
Viongozi wa Kiafrika wahimizwa kudumisha 'ujasiri' katika kushinikiza fidia ya utumwa
Dec 20, 2025 10:40Rais wa Ghana, John Dramani Mahama, amekutana na kuzungumza wajumbe wa kimataifa, lengo likiwa ni kutafuta fidia ya utumwa na ukoloni wa Wazungu katika maeneo mbalimbali ya dunia hasa barani Afrika.
-
Wanamgambo wa RSF wamewaachia huru wafanyakazi 9 wa sekta ya afya huko Darfur
Dec 20, 2025 10:33Mtandao wa Madktari nchini Sudan umeripoti kuwa wanamgambo wa Kikosi cha Msaada wa Haraka (RSF) umewaachia huru wafanyakazi 9 wa sekta ya afya waliokuwa wakishikiliwa katika magareza na kikosi hicho huko Nyala makao makuu ya jimbo la Darfur Kusini. Hata hivyo kikosi cha RSF bado kinawashikilia wafanyakazi wengine wa afya 73.
-
Iran yamnyonga ajenti wa Mossad aliyekuwa akiifanyia ujasusi Israel
Dec 20, 2025 09:32Idara ya Mahakama ya Iran imetangaza kuwa ajenti wa Shirika la Ujasusi la Israel (Mossad) aliyepatikana na hatia ya kuufanyia ujasusi utawala wa Israel, amenyongwa baada ya kukamilika kwa taratibu zote za kisheria.
-
Hamas yalaani shambulizi la kikatili dhidi ya shule katika mji wa Gaza
Dec 20, 2025 09:24Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imelaani shamulizi la kikatili la Israel dhidi ya shule moja katika mji wa Gaza lililouwa Wapalestina kadhaa. Hamas imeitaja hujuma hiyo kuwa jinai ya kivita ya makusudi na ukiukaji wa wazi wa mapatano ya kusitisha mapigano.
-
Mahakama ya Pakistan yamhukumu Imran Khan na mkewe kifungo cha miaka 17 jela
Dec 20, 2025 09:10Mahakama Maalumu ya Pakistan mapema leo Jumamosi imemhukumu Waziri Mkuu wa zamani wa nchi hiyo, Imran Khan, na mkewe Bushra Bibi kifungo cha miaka 17 jela, kila mmoja wao, katika kesi ya ufisadi inayohusiana na ununuzi wa vito vya thamani kwa bei ndogo.
-
Vikwazo vipya vya Marekani dhidi ya ICC; hujuma ya dhahir shahir inayolenga sheria na taasisi za kimataifa
Dec 20, 2025 06:40Katika hatua ya kiupendeleo ya kuuunga mkono utawala wa Kizayuni wa Israel, Marekani imewawekea vikwazo majaji wawili wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai, ICC.