-
Rais wa Zambia aidhinisha sheria ya kupanua Bunge miezi kadhaa kabla ya uchaguzi
Dec 19, 2025 03:15Rais wa Zambia, Hakainde Hichilema, jana Alkhamisi alisaini sheria ambayo itapanua Bunge la nchi hiyo, hatua ambayo wakosoaji wanasema inaweza kukinufaisha chama chake, miezi minane kabla ya uchaguzi wa kitaifa.
-
Kundi la "Hanzala" lavujisha taarifa nyeti na kudukua simu ya Naftali Bennett
Dec 19, 2025 03:00Mtandao wa al Mayadeen wa Lebanon umeripoti kuwa kundi la wadukuzi wa Iran, Hanzala, limedukua simu ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Naftali Bennett, katika operesheni iliyopelekea kuvujishwa mada nyeti na muhimu.
-
Hizbullah ya Lebanon yalaani kuvunjiwa heshima Qur'ani Tukufu nchini Marekani
Dec 19, 2025 00:05Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imelaani kwa maneno makali uhalifu na kitendo kiovu kilichofanywa na Mmarekani cha kuivunjia heshima Qur'ani Tukufu, ikielezea tukio hilo kuwa la kichochezi linalotoa harufu mbaya ya chuki, na shambulio la wazi dhidi ya matakatifu zaidi ya Waislamu na maadili ya kidini na ya kibinadamu yanayowakilishwa na dini zote za mbinguni.
-
UN: Usafirishaji bidhaa duniani kote karibuni hivi utakuwa wa kasi na wa gharama nafuu zaidi
Dec 18, 2025 23:55Usafirishaji wa bidhaa kote duniani unatazamiwa kuwa wa gharama nafuu zaidi, unaofanyika kwa kasi zaidi na kwa urahisi mkubwa, kufuatia kupitishwa makubaliano mapya yanayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa ambayo yanahuisha nyaraka zinazotumika katika usafirishaji wa kimataifa.
-
Katika kuitajirisha sekta ya silaha ya US, Qatar nayo yaomba kuuziwa ndege za F-35
Dec 18, 2025 23:55Vyombo vya habari vya Israel vimetangaza kuwa, Qatar imefanya mazungumzo na Marekani kuhusu kununua nchi hiyo ya Kiarabu ndege za kisasa za kivita za Marekani aina ya F-35.
-
Netanyahu atangaza kuidhinisha mauzo ya 'kihistoria' ya gesi ya dola bilioni 35 kwa Misri
Dec 18, 2025 23:54Waziri mkuu wa utawala wa kizayuni wa Israel, Benjamin Netanyahu ametangaza kuwa, serikali yake imeidhinisha makubaliano makubwa ya uuzaji wa gesi asilia kwa Misri yenye thamani ya karibu dola bilioni 35, akielezea kwamba makubaliano hayo ni makubwa zaidi katika historia ya Israel kwa upande wa thamani na ujazo wa usafirishaji nje.
-
Kitendo cha Waziri Kiongozi wa India kumvua Hijabu mwanamke hadharani chalaaniwa vikali
Dec 18, 2025 23:53Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International tawi la India, vyama vya siasa vya upinzani na wanaharakati mbali mbali wa ndani na nje ya nchi hiyo wamelaani vikali kitendo alichofanya Waziri Kiongozi wa Jimbo la Bihar cha kumvua niqabu hadharani daktari Muislamu katika hafla ya kiserikali iliyofanyika katika jimbo hilo.
-
Itifaki ya kimataifa kuhusu haki ya Wapalestina ya kujiainishia hatima yao
Dec 18, 2025 22:48Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) limeunga mkono haki ya Wapalestina ya kujiainishia hatima na mustakabali wao.
-
Kwa nini Uturuki haiko tayari kubadilisha misimamo yake kuhusu Gaza?
Dec 18, 2025 10:02Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki ametangaza kwamba nchi yake haitarudi nyuma na wala haitaachana na misimamo yake kuhusu Gaza.
-
UN: Zaidi ya raia 1,000 waliuawa katika shambulio la RSF Darfur
Dec 18, 2025 08:22Ripoti iliyotolewa Alkhamisi na Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema zaidi ya raia 1,000 waliuawa wakati kundi la waasi wa Sudan lilipotwaa udhibiti wa kambi ya wakimbizi wa ndani huko Darfur nchini Sudan mwezi Aprili mwaka huu.