-
Mtafiti wa Iran ashinda dhahabu katika tamasha la uvumbuzi la Silicon Valley kwa dawa ya saratani
Dec 17, 2025 23:34Mtafiti mmoja kutoka Iran ametwaa medali ya dhahabu katika Tamasha la Kimataifa la Uvumbuzi la Silicon Valley (SVIIF) 2025 huko California, Marekani kufuatia utengenezaji wa dawa bunifu inayochangia katika matibabu ya saratani.
-
Wabangladesh 32 waokolewa katika maji ya Libya
Dec 17, 2025 23:18Wahamiaji thelathini na wawili wa Bangladesh wameokolewa baada ya boti yao kuzama katika pwani ya mji wa Al-Haniya wa kaskazini mashariki mwa Libya.
-
A/Kusini yavamia kituo cha wakimbizi cha Marekani, yakamata Wakenya saba
Dec 17, 2025 23:18Kituo kimoja nchini Afrika Kusini kinachoshughulikia maombi ya visa za Marekani kimevamiwa na maafisa wa uhamiaji wa Afrika Kusini na kuwatia mbaroni raia saba wa Kenya waliokuwa wanafanya kazi nchini humo kinyume cha sheria.
-
Russia yafanya mashambulizi makubwa ya droni nchini Ukraine
Dec 17, 2025 23:16Russia imefanya mashambulizi makubwa ya ndege zisizo na rubani dhidi ya Ukraine kwa muda wa masaa kadhaa ambapo miripuko mikubwa imesikika huko Kyiv na miji mingine ya nchi humo.
-
Je, mashinikizo ya Marekani yameufanya mchakato wa uteuzi wa Waziri Mkuu nchini Iraq kuwa tata zaidi?
Dec 17, 2025 23:10Gazeti la Al-Akhbar limeandika katika ripoti yake kwamba, kuongezeka kwa mashinikizo ya kisiasa ya Marekani dhidi ya Baghdad kumeufanya mchakato wa kuunda serikali mpya ya Iraq kuwa tata zaidi.
-
Kiongozi wa Ansarullah: Waislamu wachukue hatua baada ya Qur’ani Tukufu kuvunjiwa heshima Marekani
Dec 17, 2025 09:22Kiongozi wa harakati ya Muqawama ya Ansarullah nchini Yemen amelaani vikali kitendo cha hivi karibuni cha kuvunjia heshima Qur’ani Tukufu kilichofanywa na mwanasiasa wa Marekani huku akiwataka Waislamu kote duniani kusimama imara kulinda matukufu yao.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran awaonya mahasimu kutorudia makosa ya zamani
Dec 17, 2025 09:22Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araghchi, amesema vitisho vipya vya mashambulizi ya kijeshi dhidi ya Iran ni sehemu kubwa ya vita vya kisaikolojia, akisisitiza kuwa majaribio ya awali ya kuitisha Iran kwa nguvu za kijeshi au vikwazo hayakuwahi kuzaa matokeo yaliyotarajiwa.
-
Maduro wa Venezuela aisifu Iran kama mfano wa kupigania utawala wa sheria kimataifa
Dec 17, 2025 09:20Rais wa Venezuela, Nicolás Maduro, ameitaja Iran kuwa mfano bora duniani katika kutetea sheria za kimataifa, akishukuru Jamhuri ya Kiislamu kwa msimamo wake thabiti wa kuiunga mkono Caracas wakati ambapo vitisho kutoka Marekani vinaongezeka.
-
Walimu 20 ni miongoni mwa watu 30 waliofariki baada ya boti kuzama DR Congo
Dec 17, 2025 09:19Takribani watu 30, wengi wao wakiwa walimu, wamefariki huku kadhaa wakiripotiwa kupotea baada ya boti kuzama katika mto ulioko jimbo la Kwilu, magharibi mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Kushtakiwa viongozi wa utawala wa Kizayuni; takwa la pamoja la mataifa ya Kiislamu
Dec 17, 2025 09:13Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani jinai zinazoendelea kufanywa na Israel huko Ghaza na mashambulizi yake dhidi ya Lebanon, na amezitaka nchi za ukanda huu na jamii ya kimataifa ichukue hatua kali za kukabiliana na tishio la mara kwa mara la utawala wa Kizayuni dhidi ya amani na utulivu wa eneo hili na dunia nzima kwa ujumla.