-
Ansarullah ya Yemen: Saudi Arabia inahudumia miradi ya Wamarekani-Wazayuni
Jul 19, 2026 03:24Mjumbe wa ngazi za juu wa harakati ya Ansarullah ya Yemen amesema kwamba Saudi Arabia imeweka uwezo na suhula zake za kisiasa, kifedha na kijeshi katika huduma ya miradi ya Marekani eneo la Asia Magharibi na inafanya kazi ya kudhoofisha mataifa ambayo yana misimamo dhidi ya Israel.
-
Iravani: Kutochukua hatua UN kunahalalisha haki ya Iran ya kujibu mashambulizi
Jul 19, 2026 03:20Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa, Amir Saeid Iravani, ameliandikia barua Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Katibu Mkuu wa umoja huo kufuatia uchokozi wa Marekani dhidi ya Iran, kushambuliwa miundombinu na mauaji ya raia wa Iran.
-
Ripoti: Watoto laki tano walio na umri chini ya miaka 5 nchini Madagascar wana utapiamlo
Jul 19, 2026 02:26Zaidi ya watu milioni 3.7 nchini Madagascar wanatarajiwa kukabiliwa na njaa kali huku hatari ya utapiamlo ikiongezeka miongoni mwa watoto na makundi yaliyo katika mazingira magumu.
-
UNICEF yahimiza ulinzi wa watoto wakati wa migogoro ya usalama na binadamu
Jul 18, 2026 11:51Mkuu wa Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) ametembelea kaskazini magharibi mwa Nigeria, wakati migogoro, umaskini na ukosefu wa usalama wa chakula vikiwalazimisha mamilioni ya watoto katika eneo hilo kuhitaji msaada ya dharura.
-
Op. Nasr-2: IRGC yaharibu rada ya kijeshi ya Marekani huko Kuwait katika shambulio la kulipiza kisasi
Jul 18, 2026 11:13Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) limeharibu kituo cha rada cha jeshi la Marekani katika Kituo cha Anga cha Ali Al Salem na kushambulia mkusanyiko wa wanajeshi wa nchi hiyo katika Kambi ya Arifjan huko Kuwait katika wimbi la 18 la Operesheni Nasr 2.
-
Israel yafanya mauaji makubwa huko Nuseirat, janga la binadamu linazidi kuwa baya Gaza
Jul 18, 2026 10:59Wapalestina 14 wameuawa na wengine 37 kujeruhiwa, wengi wao wakiwa katika kambi ya Nuseirat katikati mwa Ukanda wa Gaza, kutokana na mashambulizi mtawalia ya Israel yaliyolenga maeneo mbalimbali ya ukanda huo, huku hali ya kibinadamu ikizidi kuwa mbaya.
-
Kwa nini Trump Aliachana na Mpango wa Kutoza Ushuru wa 20% kwenye Lango-Bahari la Hormuz?
Jul 18, 2026 09:49Rais Donald Trump wa Marekani ameachana na mpango wake wa kutoza ushuru wa asilimia 20 kwenye Lango Bahari la Hormuz. Trump ambaye awali alidai kwamba Marekani ina nia ya kuwa "mlinzi wa Lango-Bahari la Hormuz" na kusema atatoza ushuru wa asilimia 20 kwenye njia hii ya maji ambayo hana mamlaka nayo, hatimaye ameachana na ndoto hiyo isiyothibiti.
-
WHO: Ada za mazishi zinatatiza juhudi za kudhibiti Ebola Congo DR
Jul 18, 2026 09:09Umoja wa Mataifa umeonya kwamba kusafirisha miili za waathiriwa wa virusi vya Ebola kati ya maeneo mbalimbali kwa ajili ya mazishi katika miji yao kunaweza kuchangia kuenea kwa maambukizi, wakati huu ambapo idadi ya maambukizi ya virusi hivyo imeongezeka kwa takriban 70% katika wiki mbili, huku zaidi ya maambukizi 40 mapya yakirekodiwa kila siku kwa wastani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
-
Khartoum yatoa ushahidi dhidi ya UAE na kuikosoa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai
Jul 18, 2026 09:07Waziri wa Sheria wa Sudan, Abdullah Darf, amewasilisha kifurushi cha njia za kisheria "zisizo za kawaida" ambazo serikali ya Khartoum inakusudia kuchukua ili kufungua mashtaka dhidi ya serikali ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) na kundi la waasi la Rapid Support Forces (RSF), akisisitiza kwamba Khartoum ina "ushahidi wa kutosha na data kamili" kuhusu "ushiriki wa Abu Dhabi katika vita na uhalifu uliofanywa na pande hizo mbili dhidi ya watu wa Sudan."
-
Kamanda wa IRGC aapa kuendeleza mashambulizi 'yenye ufanisi' zaidi hadi utulivu utakaporejea nchini Iran
Jul 18, 2026 03:32Mkuu wa Kikosi cha Anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) ameapa kwamba Jamhuri ya Kiislamu itaendeleza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi "yenye ufanisi" hadi utulivu utakaporejeshwa kote nchini.