Maonyesho ya "Kisiwa cha Dhambi" yafanyika Magharibi mwa Kabul
https://parstoday.ir/sw/news/world-i138538-maonyesho_ya_kisiwa_cha_dhambi_yafanyika_magharibi_mwa_kabul
Maonyesho maalumu ya yanayodhihirisha uhalifu wa nchi za kibeberu pamoja na kashfa za kingono za viongozi wa nchi za Magharibi yaliyopewa jina "Kisiwa cha Dhambi" yanafanyika magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.
(last modified 2026-05-22T04:15:54+00:00 )
May 22, 2026 04:09 UTC
  • Wamarekani wakiandamana kulaani kuhusika Trump katika jinai na ufisadi wa kimaadili katika kisiwa cha Epstein ambacho ni maarufu kama 'Kisiwa cha Dhambi'
    Wamarekani wakiandamana kulaani kuhusika Trump katika jinai na ufisadi wa kimaadili katika kisiwa cha Epstein ambacho ni maarufu kama 'Kisiwa cha Dhambi'

Maonyesho maalumu ya yanayodhihirisha uhalifu wa nchi za kibeberu pamoja na kashfa za kingono za viongozi wa nchi za Magharibi yaliyopewa jina "Kisiwa cha Dhambi" yanafanyika magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Maonyesho ya "Kisiwa cha Dhambi" yana vibanda 12 chini ya majina kama vile "Nguvu na Utawala, Usalama au Udhibiti", "Afghanistan, Miaka Ishirini ya Swali Moja", "Mafaili ya Siri", "Uadilifu au Usanii", "Elimu Chini ya Mashambulizi", "Raia, Waathiriwa wa Mstari wa Mbele" na "Wafanyakazi wa Huduma ya Afya Katika Kiini cha Mgogoro".

Mabanda hayo yanaonyesha zaidi uvamizi na mashambulizi ya nchi za kikoloni, vita, migogoro na mapigano, mauaji ya raia, pamoja na kashfa ya Epstein na kuhusika kwa baadhi ya wanasiasa mashuhuri wa nchi za Magharibi katika kesi hiyo ya kakshfa ya ngono na utovu wa maadili.

Mojawapo ya sehemu muhimu zaidi ya maonyesho hayo ni uwepo wa vijana na watoto wakiwa wameshika picha za mashahidi wa Shule ya Msingi ya Minab nchini Iran, pamoja na picha ya mjukuu wa Imam Ali Khamenei (RA) aliyeuawa shahidi katika mashambulizi ya kinyama ya Marekani na Israel dhidi ya Iran. Picha hizo zilibadilisha sura ya maonyesho kuwa mandhari ya huzuni, masikitiko na malalamiko.

Wakiwa wamebeba picha hizo, washiriki wamelaani mashambulizi ya Marekani dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na mauaji ya watoto wasio na hatia, wakitaja vitendo hivyo kuwa ni kinyume na kanuni za kibinadamu, sheria za kimataifa na maadili. Vijana walioshiriki katika maonyesho hayo wamesisitiza kwamba hawatasahau uhalifu dhidi ya watoto na mauaji ya wanafunzi wasio na hatia nchini Iran.