-
Oman yaunga mkono mpango wa Iran wa kutoza ‘ada za huduma’ katika Lango la Hormuz
Jun 30, 2026 11:27Waziri wa Mambo ya Nje wa Oman, Badr al-Busaidi, ametangaza msimamo wa nchi yake kuunga mkono mpango wa Iran wa kuanzisha utaratibu wa “ada za huduma za baharini” kwa meli zinazopita katika Lango Bahari la Hormuz.
-
Jeshi: Mazishi ya Kiongozi Shahidi yatakuwa mwamko wa kimataifa dhidi ya ugaidi na jinai za Marekani na Uzayuni
Jun 30, 2026 11:23Jeshi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limesema kuwa sherehe za kitaifa za kuaga na mazishi ya Kiongozi Shahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, zitatumika kama jukwaa la harakati za kimataifa za kulaani ugaidi na maandamano hai dhidi ya jinai zinazofanywa na mhimili wa Marekani na Uzayuni.
-
Mjumbe wa Palestina ataka jumuiya ya kimataifa izuie hatua za Israel za kupora ardhi ya Palestina
Jun 30, 2026 11:21Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa ameitaka jamii ya kimataifa kuacha kauli za kulaani pekee na badala yake kuchukua hatua za kivitendo ili kusitisha mpango wa Israel wa kupora ardhi za Palestina.
-
Polisi wa Afrika Kusini wakabiliana na waandamanaji wanaopinga wageni
Jun 30, 2026 11:18Mamlaka nchini Afrika Kusini zimeimarisha ulinzi kwa kupeleka vikosi vya polisi katika miji mikuu ya nchi hiyo, kufuatia wimbi la maandamano dhidi ya raia wa kigeni wasio na nyaraka rasmi za ukaazi.
-
Kwa nini makubaliano ya Washington yamefungua njia ya fitina mpya nchini Lebanon?
Jun 30, 2026 05:53Nabih Berri, Spika wa Bunge la Lebanon ametahadharisha kuhusu njama mpya dhidi ya Lebanon akiashiria makubaliano ya Washington kati ya serikali ya Lebanon na utawala wa Kizayuni wa Israel na kuwahutubu wananchi wa nchi hiyo kwa kusema: "Enyi watu wa Lebanon, hii ni njama hatari."
-
Pezeshkian: Dola bilioni 6 za Iran zinazozuiwa Qatar kuachiliwa
Jun 30, 2026 03:51Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Masoud Pezeshkian, ametangaza kuwa kiasi cha dola bilioni 6 mali ya nchi hii zinazozuiliwa Qatar kufuatia mashinikizo ya Marekani, zitaachiliwa.
-
Hamas: Kimya cha dunia kuhusu watoto wa Kipalestina waliouawa Gaza ni kushiriki katika mauaji ya kimbari ya Israel
Jun 30, 2026 03:46Katika taarifa yake Jumatatu usiku, msemaji wa Hamas, Hazem Qassem, alisema kwamba mtoto wa Kipalestina asiye na hatia aliyeuawa jana na jeshi la Israel ndiye mwathirika wa hivi karibuni zaidi miongoni mwa makumi ya maelfu ya watoto wa Kipalestina waliouawa katika mashambulizi ya mabomu ya Wazayuni, njaa, kunyimwa huduma za matibabu, ugaidi na kutokana na huzuni ya kufiwa na wazazi wao.
-
Ghasia dhidi ya wahamiaji Afrika Kusini zatarajiwa leo
Jun 30, 2026 03:42Afrika Kusini inakabiliwa na mtihani mkubwa wa kiusalama baada ya magenge ya wahalifu kuapa kuwatimu raia wa kigeni nchini humo kuanzia leo.
-
Korea Kaskazini yaituhumu Japan kujigeuza ‘Taifa la Vita’ kufuatia mazoezi ya kijeshi na Marekani
Jun 30, 2026 03:40Korea Kaskazini imekosoa vikali mazoezi ya kijeshi yanayoendelea kati ya Marekani na Japan, ikiituhumu Tokyo kutumia hali ya sasa ya dunia iliyojaa misukosuko kama kisingizio cha “kujihalalishia mabadiliko yake kuwa taifa la vita.”
-
Wasomi wanawake wa Iran wataka Marekani na Israel ziwajibishwe kwa jinai zao
Jun 30, 2026 03:27Kundi la wanazuoni wanawake wa Iran, wasomi wa taaluma mbalimbali na wataalamu wa masuala ya utamaduni, limesambaza barua ya wazi likirekodi ukiukaji wa kimfumo uliofanywa na Marekani na Israel wakati wa vita vya hivi karibuni dhidi ya Iran, na limetoa wito kwa jamii ya kimataifa kuchukua hatua za dharura za uwajibikaji.