-
Iran: Marekani ina jukumu la kuhakikisha inakomesha kabisa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon
Jun 16, 2026 11:14Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Abbas Araghchi amesema kuwa Marekani ina jukumu la kuhakikisha utekelezwaji wa hati ya maelewano (MoU) ya makubaliano itakayosainiwa na Tehran na Washington ikijumuisha kusitishwa mashambulizi ya Israel dhidi ya Lebanon.
-
Mkuu wa Jeshi la Iran: Adui yeyote atakayefanya makosa atakabiliwa na ghadhabu kubwa
Jun 16, 2026 11:09Kamanda Mkuu wa Jeshi la Iran amesema adui alishindwa kufikia malengo yake yoyote kupitia vita viwili, akionya kwamba makosa yoyote ya kimahesabu yatakabiliwa na hasira kali ya Jeshi la Iran.
-
Wapiganaji wa Hizbullah wakabiliana na wanajeshi vamizi wa Israel kusini mwa Lebanon
Jun 16, 2026 11:07Wapiganaji wa Hizbullah wakabiliana na wanajeshi vamizi wa Israel kusini mwa Lebanon
-
Kesi inayomkabili wa Rais wa zamani wa CAR yaanza kusikilizwa bila ya yeye kuwepo mahakamani
Jun 16, 2026 11:06Kesi inayomkabili aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Francois Bozize, imeanza kusikilizwa katika Mahakama Maalumu inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.
-
Nigeria: Karibu wapiganaji 10,000 wa zamani wa Boko Haram waunganishwa katika jamii
Jun 16, 2026 11:00Mamlaka husika katika Jimbo la Borno kaskazini mashariki mwa Nigeria zimearifu kuwa karibu wapiganaji 10,000 wa zamani wa kundi la waamgambo wa Boko Haram sasa wameunganishwa tena katika jamii chini ya mpango unaofadhiliwa na serikali wa kurekebisha tabia na kuhimiza kuachana na makundi ya uasi.
-
Marekani ilishindwa vipi katika vita dhidi ya Iran?
Jun 16, 2026 06:29Siku mia moja na sita baada ya kuanza hujuma za kijeshi za Marekani na Wazayuni dhidi ya Iran, hatimaye Tehran na Washington zimefikia muafaka katika mfumo wa makubaliano ya kuhitimisha rasmi vita hivyo.
-
Iran yatoka sare ya mabao 2 kwa 2 na New Zealand, Misri yagawana pointi na Ubelgiji Kundi G
Jun 16, 2026 05:53Timu ya Taifa ya Iran, Team Melli, imetoka sare ya mabao mawili kwa mawili na timu ya taifa ya New Zealand katika mechi ya kundi G iliyopigwa uwanja wa SoFi Stadium huko California.
-
Pezeshkian: Hasira ya Israel dhidi ya MoU na Marekani ni 'ishara dhahiri' ya ushindi wa Iran
Jun 16, 2026 03:23Rais Masoud Pezeshkian wa Iran amesema hasira ya Israel kuhusu hati ya maelewano (MoU) ya makubaliano kati ya Iran na Marekani inaashiria wazi mafanikio na ushindi wa taifa la Iran.
-
Ayatullah Amoli Larijani: Istiqama ya taifa imeshinda 'kiburi kibaya cha US-Israel
Jun 16, 2026 02:59Mkuu wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesifu istiqama na ushujaa wa taifa kubwa la Iran mbele ya "kiburi kibaya" cha Marekani na utawala wa Israel.
-
Waziri Mkuu: Pakistani itakuwa mwenyeji wa hafla ya "kihistoria" ya kusaini makubaliano ya Iran na Marekani mjini Geneva, Juni 19
Jun 16, 2026 02:57Waziri Mkuu wa Pakistani, Shehbaz Sharif amesema kuwa hafla ya kutia saini Mkataba wa Maelewano kati ya Iran na Marekani (MOU) itaandaliwa na nchi yake mjini Geneva, Juni 19 mwaka huu.