-
Jinai mpya: Hamas yailaani Israel kwa kufukua mamia ya makaburi huko Gaza
Jan 28, 2026 04:08Harakati ya muqawama ya Palestina, Hamas, imelaani jinai mpya ya utawala mhalifu wa Israel, ikisema kuwa wanajeshi wa Israel wamefukua mamia ya makaburi katika eneo la mashariki la Ukanda wa Gaza unaozingirwa. Wanajeshi wa utawala wa Kizyauni wamefukua makaburi ya Wapalestina wakitafuta mwili wa mateka wa mwisho wa utawala huo.
-
MONUSCO yawarejesha nyumbani waasi 15 wa zamani wa Rwanda kutoka Kongo
Jan 28, 2026 04:00Kikosi cha Kulinda Amani cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (MONUSCO) kimeripoti kuwa kimewarejesha nyumbani Wanyarwanda 34, wakiwemo wapiganaji 15 wa zamani wa kundi la waasi la Democratic Forces for the Liberation of Rwanda (FDLR).
-
Kenya katika kivuli cha ukoloni wa Uingereza; simulizi ya umwagaji damu na ukandamizaji dhidi ya Mau Mau
Jan 28, 2026 02:07Katika miaka ambayo Uingereza ilijiona kuwa taifa kubwa na lisilo na mpinzani duniani, ardhi moja katika Afrika Mashariki polepole ikageuka na kuwa eneo la mojawapo ya uzoefu mchungu zaidi wa kikoloni.
-
Rais Pezeshkian: Vita vya kisaikolojia vya Marekani vinalenga kuvuruga usalama Asia Magharibi
Jan 28, 2026 00:59Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, ameonya kwamba harakati za kijeshi za Marekani katika Asia Magharibi ni sehemu ya juhudi zilizopangwa za kuyumbisha amani ya eneo hilo.
-
The Guardian: Hofu inayotanda Minneapolis inafanana na ya vita vya wenyewe kwa wenyewe
Jan 28, 2026 00:59Makala ya uchambuzi iliyochapishwa na gazeti la Uingereza la The Guardian imefafanua ilichokielezea kuwa ni eneo la kutisha huko Minneapolis, Minnesota, nchini Marekani na kusema kwamba ni wakati muhimu unaofichua sura ya ufashisti wa wazi chini ya utawala wa Rais Donald Trump.
-
Jeshi la Sudan lavunja mzingiro wa miaka 2 wa wanamgambo wa RSF dhidi ya mji muhimu huko Kordofan
Jan 28, 2026 00:58Jeshi la Sudan limeeleza kuwa limevunja mzingiro wa karibu miaka miwili wa wanamgambo wa RSF katika mji muhimu katika mkoa wa Kordofan, na kudhibiti njia kuu za usafirishaji.
-
Somalia yakamata msaada wa chakula uliorejeshwa kwa WFP baada ya kutoelewana na Marekani
Jan 28, 2026 00:57Serikali ya Somalia imesema kuwa msaada wa chakula uliotolewa kwenye ghala wakati wa shughuli za upanuzi wa bandari katika mji mkuu, Mogadishu, umerejeshwa kwa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), kufuatia ripoti kwamba maafisa wa eneo hilo wamekamata msaada wa chakula uliotolewa na nchi wafadhili.
-
Polisi 10 wauawa katika shambulio kwenye kituo cha polisi Niger
Jan 27, 2026 23:01Askari polisi wasiopungua 10 wa Niger wameuawa wakati watu wenye silaha waliposhambulia kituo cha polisi kaskazini mwa nchi hiyo. Eneo la kaskazini mwa Niger limekumbwa na machafuko ya magenge ya wahalifu wenye silaha.
-
Baqaei: Kampeni ya kueneza uongo dhidi ya Iran imefichuliwa
Jan 27, 2026 10:07Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran mapema leo ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X, akionyesha video iliyorushwa hewani na Channel 12 ya Israel ambapo mwanamke Muisraeli anashangazwa na tangazo la picha yake akitajwa kuwa ni miongoni mwa "waliouawa" katika maandamano nchini Iran.
-
Uganda inapanga kuwaondoa wanajeshi wake katika kikosi cha kulinda amani Somalia
Jan 27, 2026 10:06Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, amesema nchi yake inapanga kuondoa wanajeshi wake huko Somalia baada ya kuwepo huko kwa kipindi cha miaka 19.