Oct 15, 2023 15:20 UTC
  • Umoja wa Mataifa watoa wito wa kulindwa Mashia nchini Afghanistan

Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Haki za Binadamu ametoa wito wa kulindwa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Afghanistan.

Richard Bennett ametoa wito huo kufuatia mashambulizi ya kigaidi yaliyofanywa dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia waliokuwa wakitekeleza ibada katika Msikiti wa Imam Zaman (AS) katika Mkoa wa Baghlan.

Kwa mujibu wa duru za ndani, waumini 30 waliuawa shahidi na karibu wengine 50 walijeruhiwa katika hujuma ya kigaidi iliyolenga Msikiti wa Imam Zaman (AS) katika mji wa Pul Khumri, mji mkuu wa Mkoa wa Baghlan, Afghanistan.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Afghan Sauti ya Afghanistan (AVA), Richard Bennett, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa Kuhusu Haki za Binadamu, ameandika ujumbe kwenye mtandao wa kijamii wa X akisema: "Kinga, ulinzi na uwajibikaji vinahitajika kwa jamii ya Mashia wa Afghanistan, ambao wanaendelea kushambuliwa. kuwa walengwa." Bennett amelaani shambulizi hilo la kigaidi na kutoa rambirambi zake kwa familia za wahasiriwa.

Mapema jana Kundi la kigaidi la Daesh lilitangaza kuhusika na hujuuma iliyofanyika katika Msikiti wa Imam Zaman (A.S) huko Pul--Khumri makao makuu ya jimbo la Baghlan kaskazini mwa Afghanistan.

Tags